Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwigizaji na mwanamziki,  Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ambae ni mama wa watoto wawili wa kike , akiwa na mchumba wake Nuh wamechafua hali ya hewa baada ya kutupia picha yao inayowaonyesha wakiwa watupu.
Nuh Mziwanda ndio alioibandika picha hiyo kwenye ukursa wake kwenye mtandao wa instagram na baada ya kuona wengi wanamshabulia aliamua kuibandua. Kwa kiufupi picha hii haina maadili na ukizingatia mwanadada Shilole ni mama na sijui watoto wake watajifunza nini hapa.
Wapo walioona kuwa kitendo hiki alichokifanya Mziwanda labda ni kutokana na umri wake hivyo hayo ni baadhi ya matokeo ya kuwa na mahusiano  na mtu mtoto mdogo  na kuona Mziwanda hana kosa hapa. Lakini pia wapo walioona kuwa wawili hawa wanatafuta KIKI tu ili media za hapa Bongo ziwazungumzie kama Zari na Diamond, ila pia wapo amabo wanaona hii ipo poa  na haina tatizo.
Nadhani kitendo cha Mziwanda kubandua picha hii ni kutokana na akili yake ku-CLICK kuwa amekosea, nampongeza kwa hilo na naamini atakuwa amejifunza kitu.
Nia na madhumuni ya kuileta hapa ni kutaka watu watambue kuwa mtandao ni zaidi ya tunavyofikilia kwani kosa la sekunde moja mtandaoni linaweza kukuhalibia maisha yako yote..Siku nyingine naamni watakuwa makini.
Mzee wa Ubuyu

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top