Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Habari  Bongomovies, Kwanza kabisa nawapongeza kwa kutupa fursa  na sisi mashabiki wenu kuweza  kutoa yetu ya moyoni kuhusu tasnia yenu ya filamu.
Kwanza kabisa mimi ni mshabiki namba moja kabisa wa “madame” (Wema Sepetu) tangu akiwa Miss na alipoingia kwenye tasina ya filamu ndipo nimezidi kumpenda zaidi, nimekuwa ni moja kati ya followers wake kwenye mitandao yote ya kijamii na zaidi huwa sikosi ile show yake ya “In My Shoes” nimeanza hiyo ili niweze kueleweka vizuri.
Swali langu kwa madame ni kwamba ile filamu  ya “DAY AFTER DEATH” (D.A.D) aliyomshirikisha muigizaji kutoka nchini Ghana, Van Vicker inatoka lini?.
Kama kukumbukumbu zangu zipo vizuri , mwishoni mwa mwaka jana madame alikwenda nchini Ghana  nakukutana na mwigizaji Van Vicker  ambako walisema wanatengeneza filamu itakayo kwenda kwa jina la Day After Death na kutuaidi kuwa itatoka muda sio mrefu.
Kitu ambacho nilifarijika nakumpongeza sana  madame kwenye  mitandao , sio kwasababu tu nampenda na kumkubali bali niliona amefanya jambo zuri la kuvuka mipaka, sasa  wasiwasi na mashaka yangu ni kwamba mbona hadi leo hii kimya, hata kusikia kuwa itatoka lini?.
Tafadhari madame naomba utujuze, au tuamini kuwa ilikuwa ni PROJECTIIII tu?.
Asanteni.
By Emily Juma

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top