Watu wanaolala kwa zaidi ya masaa
manane kwa siku wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa
kiharusi,utafiti umesema lakini wataalam hawajua sababu yake.
Utafiti
uliofanywa kwa takriban watu 10,000 katika chuo kikuu cha Cambridge
ulibaini kwamba wale wanaolala kwa takriban saa nane wana uwezekano
mkubwa wa asilimia 46 kupata kiharusi.Watu wazima hupendelea kulala kati ya saa sita na tisa ili kupumzika vizuri,lakini kulala zaidi hushirikishwa na matatizo ya afya kama vile ugonjwa wa sukari pamoja na ule wa kunenepa kupitia kiasi.
Hatahivyo haijabainika kutoka kwa utafiti huo iwapo kulala kwa zaidi ya saa nane huenda ndiko kunakosababisha matatizo hayo ambayo husababisha kiharusi ama iwapo ni miongoni mwa sababu za magonjwa yasiojulikana.
Utafiti huo ulifanywa miongoni mwa watu walioko na kati ya miaka 42 na 81.
Post a Comment