Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This



Na Emanuel Madafa,Mbeya

Waziri Mkuu Mheshimiwa  Mizengo Pinda anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya  siku Nane Mkoa wa Mbeya ambayo itahusisha  Halmashauri saba za Mkoa huo.

Katika ziara hiyo Mheshimiwa Waziri Mkuu atatembelea halmashauri Saba  za Mkoa huo ambazo ni Halmashauri ya jiji la Mbeya ,Kyela,Busokelo Rungwe ,Mbozi pamoja na Chunya kuaznia Feb 23 hadi Machi 1 mwaka huu..

Akizungumza jijini mbeya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amesema Lengo la Ziara hiyo ni kukagua miradi  mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali halmashauri pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo katika mkoa wa mbeya.

Amesema  katika Ziara hiyo Waziri Pinda atakagua  na kuweka mawe ya msingi pamoja na kuzindua miradi katika sekta ya Elimu ,Afya ,Ujenzi Barabara kilimo na umwagiliaji maji masoko na hifadhi ya chakula.

Aidha amesema  Waziri Mkuu atapata fursa ya kuhutubia mikutano ya hadhara ambayo itafanyika katika kila Halmashauri husika katika ziara hiyo.

Pia amewataka wananchi wa mkoa wa mbeya kuendelea kudumisha amani na utulivu katika  siku zote Nane za ziara ya Waziri Mkuu ambapo amewahakikishia wananchi kuwa serikali imejipanga vyema katika kuhakikisha mkoa unakuwa salama katika kipindi hicho.
Mwisho..

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top