Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na Wakandarasi
wanaojenga mradi Maji Safi na Maji Taka Mjini Sumbawanga ambao ni Techno
Fab na Mkandarasi mshauri GKW ambapo amewataka kuongeza kasi kumaliza
mradi huo ambao upo nyuma ya wakati. Amemuagiza Mkandarasi anaejenga
kukamilisha ujenzi huo kwa kipindi cha miezi miwili ijayo licha ya
kuomba kuongezewa muda wa miezi sita ili aweze kukamilisha kazi hiyo.
Alisema
kuwa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ni lazima uende na wakati
kuhakikisha huduma muhimu zinawafikia wananchi kwa wakati na hivyo
kupisha malalamiko ya wananchi kwa Serikali yao. Kwa upande mwingine
ameuagiza uongozi wa Maji Safi na Maji Taka Mjini Sumbawanga kumfikishia
taarifa za Mkandarasi Herken Builders Ltd aliyojenga mradi wa maji wa
visima nane na "pumps" ambazo hazifanyi kazi aweze kumchukulia hatua
stakihi ikiwepo kumuandikia barua kuwa hastahiki kufanya kazi katika
Mkoa wake wa Rukwa.
|
Post a Comment