Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Msafara wa watu 25 wa timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) unatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam siku ya alhamis, kabla ya kuunganisha ndege siku ya ijumaa kuelekea jijini Mwanza tayari kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Taifa Stars siku ya jumapili.

Katika msafara huo utakaokuwa na wachezaji 18 na viongozi 7, kocha mkuu wa The Flames Young Chimodzi amewajumuisha wachezaji nane (8) katika kikosi chake wanaocheza soka la kulipwa katika nchi za Afrika Kusini, Congo DR, Msumbuji na Zimbabwe.

Wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini ni Limbikani Mzava (Celtic), Harry Nyirenda (Black Leopards), Esau Kanyenda (Polokwane City), na Atusaye Nyondo (University of Pretoria).

Wengine ni Nahodha Joseph Kamwendo (Tp Mazembe - Congo DR), Frank Banda (HBC Songo - Msumbuji), Chimango Kayira (Costal De Sol - Msumbuji) na Gerald Phiri (Caps United - Zimbambwe).


VPL KUENDELEA KESHO
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ianatrajiwa kuendelea kesho (jumatano) kwa mchezo mmoja kupigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, kwa wenyeji JKT Ruvu kuwakaribisha vinara wa ligi hiyo timu ya Young Africans.

KILUVYA BINGWA SDL
Timu ya Kiluvya United ya mkoa wa Pwani jana imetawazwa Mabingwa wapya wa Ligi Daraja la Pili (SDL) baada ya kuifunga Mbao FC ya Mwanza kwa mabao 4-2 katika mchezo wa fainali uliofanyika kwenye Uwanja wa kumbukumbu ya Karume jijini Dar es salaam.

Kiluvya United inaunganana timu za Mji Mkuu (CDA) ya Dodoma, Mbao FC ya Mwanza na Mji Njombe ya Njombe kupanda Ligi Daraja la Kwanza (FDL)msimu ujao, huku timu za Ujenzi Rukwa, Katavi FC na Volcano zikishuka daraja kutoka Ligi Daraja la Pili.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top