Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Meneja wa Mauzo kampuni ya Mohamed Enterprises .Co.ltd tawi la mbeya Ndugu Peter Mkumbukwa  (37) mkazi wa mbeya  amefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria lenye namba za usajili T.784 Dca aina ya shandon lililokuwa likiendeshwa na dereva aitwaye Juma Alukamba kuligonga kwa nyuma gari T.928 CKK aina ya fuso. likiendeshwa na dereva lifu mahenge.

Ajali hiyo ilitokea Machi  25 ,2015 majira ya saa 8  mchana huko katika eneo la kijiji cha Idweli, kata ya isongole, , wilaya ya rungwe, mkoa wa mbeya katika barabara kuu ya mbeya/tukuyu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi amesema  katika ajali hiyo, dereva wa gari lenye namba T.784 DCA Juma Alukamba alijeruhiwa na amelazwa katika hospitali ya misheni Igogwe.

Amesema chanzo  cha ajali hiyo  ni mwendo kasi wa gari namba T.784 dca ambapo mara baada ya jail hiyo  Dereva wa fuso  alikimbia, huku juhudi za kumtafuta zinaendelea.

Aidha  Msangi  anatoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria/kanuni na alama za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.

 MWISHO


Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top