Na Saimeni Mgalula,Mbeya
Wakala wa Usafirishaji na uuzaji wa Magari Madogo ndani na
nje ya Tanzania kutoka katika kampuni ya Yard iliopo maeneo ya Chapwa katika
Mji wa Tunduma Uliopo Wilayani Momba Mkoani hapa,Emanuel Msolopa,amekichangia
kikundi cha sanaa za Filamu cha Momba arts Group Shilling Laki saba.
Akizungumza katika uzinduzi wa filamu ya Police story hivi karibuni katika Tafrija
ya Uzinduzi wa Filam yao inayo iitwa Police Story iliyofanyikia katika ukumbi wa Highclass Hotel
iliopo katika mji wa Tunduma .
Alisema aliwataka Waigizaji hao kuacha kasumba ya
kuwanyenyekea wasanii wakongwe wa filamu
kutoka sehemu mbalimbali kwa lengo la
kuwataka wajiami na ndio wao watafutwe na wasanii wakubwa na sio wao kuwatafuta
wasani wakongwe alisema Msolopa
Msolopa alisema kapuni
ya Yard ipotayari kuwasaidia wasanii wa filamu wa mikoani hasa mkoa wa Mbeya
ambapo ndio kuna yard hiyo na haya
aliyasisitizia sana kwa wasanii wa Wilayah ii hasa walipo katika kikundi hicho
ambacho kinakuja kwa kasi ,alisema wakala huyo.
Wakala huyo alisema kutokana na Risala aliyosomewa akiwa
kama mgeni Rasmi kwa madai ya kwamba Filamu hiyo mpaka kukamilika imegharimu
shilling Milioni Tano na ilifilamu hiyo isambaye nchi nzima wanahitaji shilling
milioni 20.
‘’Mara baada ya kusomewa alisema ili kuweza kupata fedha
hizo inatubidi kila baada ya miezi sita wawe wanaweka Tamasha kubwa katika
kumbi tofauti tofauti za hapa Mkoani ili wawe wanaonyesha vipaji vyao na sio
kukaa tu na kusubiri mpaka mtakapo
uza,’’
Aliongezea kwa kuwahaidi kuwa kama wataongeza bidii yeye
yupo tayari kupeleka maombi kwa wakubwa wa kampuni yao ili waweze kupata
mzamini kutoka katika kampuni hiyo ya yard pindi watakapo onyesha nia.
Mbali na hayo mmoja kati ya Wachezaji wa Filamu hiyo Boni
Bernad alosema kuwa lengo kubwa la kuanzisha
kikundi cha sanaa ni kulimisha jamii kwa njia ya sanaa hata kama kunachangamoto
nyingi katika kazi yeyote lakini wao
wapo tayari kupambana ,alisema hiyo mmoja huyo
Mwisho
Post a Comment