Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwigizaji  mkongwe katika tasnia ya filamu,  Novatus Mayenja ‘Nova’ amedai kuwa wasanii wengi wa filamu ni mafukara wa mawazo na hawajui wafanyalo ndio sababu ya kuwafanya washindwe kujijenga kimaisha kwani hawana muda wa kutafuta maisha ya kweli.
“Mimi nasema kuwa wasanii wengi ni mafukara wa mawazo, hawajitambui, hawajui nini wanahitaji zaidi ya ubishoo, mtu akiwa na kagari kamkopo hata deni hajamaliza, lakini mtu anajitutumua na kujiona kama bilionea,”anasema Nova.
Msanii huyo mwenye mbwembwe anasema kuwa kulingana na maisha yalivyo ni vema wasanii wakajitaidi kujenga nyumba zao kuliko maisha ya sasa ya kununua magari huku wakiishi nyumba za kupanga na magari yao kuyalaza sehemu  kwani ni mengi hayatoshi walipopanga.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top