MWENDESHA PIKIPIKI AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI CHUNYA.
MTU MMOJA MKAZI WA IDIMI JIJINI MBEYA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA AKIWA NA MICHE 08 YA BHANGI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA AMBAYE HAKUWEZA
KUFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, JINSI YA KIUME, UMRI KATI YA MIAKA 35 –
40 ALIKUTWA AMEUAWA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA NA MWILI WAKE UKIWA
UMETELEKEZWA NDANI YA MTO MOMBA.
MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA MNAMO
TAREHE 29.03.2015 MAJIRA YA SAA 08:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOJI,
KIJIJI, KATA NA TARAFA YA KAMSAMBA, WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA. MWILI
WA MAREHEMU ULIKUTWA UKIWA UMEHARIBIKA SANA HUKU UKIWA NA MAJERAHA YA
KUKATWA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU YA KICHWANI, MIGUUNI, KIFUANI NA
TUMBO KUPASUKA. CHANZO CHA TUKIO KINACHUNGUZWA.
JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MWENDESHA PIKIPIKI MMOJA AMBAYE
HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, UMRI KATI YA MIAKA 25 – 30
ALIYEKUWA AKIENDESHA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.519 CRD AINA YA
T-BETTER ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI
LISILOFAHAMIKA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA
MAKAZI YAKE.
AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE
29.03.2015 MAJIRA YA SAA 21:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA ISENYELA,
KATA YA MBUGANI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA
KATIKA BARABARA YA MBEYA/CHUNYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA
WA GARI ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA AJALI. JUHUDI ZA KUMTAFUTA
ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA MATUKIO HAYO AZITOE KATIKA
MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI
YAO.
TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA, JESHI LA
POLISI MKOANI MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA IDIMI ALIYEFAHAMIKA
KWA JINA LA MICHAEL JONAS (35) AKIWA NA MICHE NANE [08] YA BHANGI
ALIYOPANDA ENEO LA NYUMBA YAKE.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
29.03.2015 MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA IDIMI, KATA
YA IHANGO, TARAFA YA TEMBELA, WILAYA YA KIPOLISI MBALIZI, MKOA WA MBEYA.
TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME
CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment