Baadhi ya vitu mbalimbali vikiwa vimewekwa nje ya baada ya moto wa ajabu kuibuka na kuteketeza nyumba eneo la Mtaa wa Mageuzi Kata ya Nsalala Mbalizi Mbeya. |
waathirika wa moto huo wakiwa wahajui nini cha kufanya mara baada ya moto huo wa ajabu kuibuka |
Moto huo wa ajabu ukiwa umeunguza ukuta licha vitu kutolewa nje |
Na Ezekiel Kamanga ,Mbeya
Mkazi
wa mtaa wa mageuzi kata ya Nsalala Mbalizi Mbeya Bi Tatu Hatibu miaka (40)
amelazimika kulala nje ya nyumba yake akiwa na wafamilia yake ya watu 8 baada
ya nyumba yake kukumbwa kadhia ya moto wa ajabu.
Tukio
hilo la ajabu lilianza kutokea alfajiri ya jumatatu wiki hii ambapo moto ulianza kuwaka
katika moja ya vyumba wanavyolala watoto ambapo moto huo uliteketeza magodoro
wakati watoto wakiwa wamelala.
Jambo
la kushangaza katika tukio hilo ni magoro na nguo kuteketea kwa moto huku miili
ya binadamu waliokuwa wamelala kwenye magodoro hayo kutopata madhara yoyote.
Akielezea
mkasa huo Bi Tatu ambaye ni mwathirika
wa tukio hilo amesema tukio hilo limekuja siku chache baada ya kushinda kesi
dhidi ya jirani yake ambayo iliamriwa katika mahakama ya Mbalizi.
Amesema
kesi hiyo ilikuwa inahusu ungomvi wa makazi yeye pamoja jirani yake ambapo
katika eneo analo ishi bibi huyo kulikuwa na kipande cha ukuta ambacho
kiliongezeka kujengwa hadi eneo la nyumba yake hali ambayo iliibua mgogoro huo.
Nao
baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo ambao ni familia ya Bi.TATU wamesema kutokana
na kadhia hiyo hivi sasa wamelazimika kulala nje ya nyumba yao kukwepa maafa
zaidi.
Blog
hii imeshuhudia familia hiyo ikiwa nje
ya nyumba yao kwa kuofiwa kukutwa na maafa zaidi ambapo hadi tunakwenda
mitamboni bado moto huo uliendelea kuteketeza baadhi ya vitu katika makazi ya
Bibi huyo..
Post a Comment