Na Baraka Kizuguto,Dar es Salaam
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu wa nchini TFF, Jamal Malinzi amewatakia kila la
kheri wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye kombe la Shirikisho barani Afrika
(CC) Young Africans, katika mchezo wa marudiano dhidi ya FC Platinum ya
Zimbabwe utakochezwa siku ya jumamosi kwenye uwanja Mandava uliopo Gweru
Bulawayo.
Malinzi
amesema Young Africans hawapaswi kubweteka na ushindi walioupata awali wa mabao
5-1, kikubwa wanapaswa kwenda kupambana kusaka ushindi ugenini ili kuweza
kufuzu kwa hatua inayofuata ya timu 16.
Endapo
Young Africans itafanikiwa kuwatoa FC Platinum itaingia katika hatua ya 16 bora
na itakutana na mshindi kati ya timu za Benifica de Luanda ya Angola au Etoile
du Saleh ya Tunisia
Wakati huo huo timu
ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) ijumaa ya tarehe 10,
Aprili mwaka huu, itashuka dimbani Uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam kuwakarisbisha timu ya Taifa ya Wanawake ya Zambia (The She-Polopolo).
Twiga
Stars inayonolewa na kocha mkuu Rogasian Kaijage iliingia kambini mwishoni mwa
wiki na kikosi cha wachezaji 25 katika hostel za TFF zilizopo Karume, kujiandaa
na mchezo huo ambao ni muhimu wa kuwania kufuzu kwa fainali za michezo ya
Afrika mwaka huu.
Katika
mchezo wa awali uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini Lusaka Zambia, Twiga
Stars iliibuka na ushindi wa mabao 4-2, mabao yaliyofungwa na Asha Rashid (2),
Shelder Boniface (1) na Sophia Mwasikili (1).
Mshindi
wa jumla katika mchezo huo atafuzu moja kwa moja kwa fainali za Michezo ya
Afrika zitakazofanya nchini Congo - Brazzavile kuanzia Septemba 13 mwaka huu.
Mwisho.
Post a Comment