Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
nchini TFF, Jamal Malinzi leo amefungua kozi ya walimu wakufunzi wa mpira wa
miguu chini inayofanyika katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
Malinzi amesema kozi hiyo ni muhimu
kwa mustakabali wa soka la Tanzania, walimu wakufunzi watasaidia kuwafundisha
walimu wengine wa mpira, ili kuweza kufundisha mpira kwa watoto wadogo ambao
ndio hazina ya baadae.
Malengo ya TFF ni kuhakikisha timu ya
vijana ya U17 inafuzu kwa fainali za Mataifa Afrika 2017 nchini Madagscar, na
baadae kuwa na kikosi bora wakati tunapotarajia kuwa wenyeji wa fainali za U17
Afrika mwaka 2019 "alisema Malinzi".
TFF ina program mbili za kuwaandaa
vijana wenye umri chini ya miaka 13, 15 kwa kuwaweka kambini na kucheza michezo
ya kirafiki mikoani na kufanya ziara katika nchi za Malawi, Zambia, Zimbabwe,
Bostwana na Afrika Kusini.
Aidha Malinzi amewaomba walimu
wakufunzi kuwa karibu na makocha wa timu za Taifa, na kuwapa ushauri makocha
hao ili kuweza kuwasaidia katika kuboresha vikosi vyao na maendeleo ya soka la
Tanzania kwa ujumla.
Naye Rais wa CECAFA na Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji ya CAF, Leodgar Tenga alimshukuru Malinzi kwa kuweza
kufungua kozi hiyo ambayo inawakutansisha walimu wakufunzi wa mpira miguu
kutoka sehemu mbalimbali nchini.
Akiongea kwa niaba wa walimu wakufunzi, Dr.
Mshindo Msolla alisema wanaishukuru TFF kwa kuandaa kozi na kuomba kuendelea
kushirikishwa katika mipango mbalimbali ya soka nchini ikiwa ni pamoja na
kutambulika kuanzia katika ngazi za juu mpaka katika maeneo waliyopo.
Kozi hiyoiliyoanza leo jumatatu
itamalizika Mei 2 mwaka huu, inawajumuisha walimu 18, wenye leseni A, B na C za
CAF kutoka mikoa mbalimbali Tanzania bara na Zanzibar.
mwishoo.
Post a Comment