Wataalam wa masuala ya uchumi
wamesema kuwa China inakabiliwa na wimbi la kushuka kwa ukuaji wa uchumi
wa taifa hilo la pili duniani katika kasi ya kukua kiuchumi.
Kiwango
cha ukuaji wa uchumi wa taifa hilo kwa mwaka cha asilimia saba katika
miezi mitatu ya mwanzo,ikilinganishwa na miezi hiyo hiyo mwakajana
inaonyesha kushuka kwa kasi ya ukuaji wa uchumi wa China katika miaka
sita mfululizo.
Serikali ya China inadaiwa kupunguza kasi ya
ukuaji wa uchumi wa taifa lake ili kuendana na malengo ya muda mrefu ya
taifa hilo katika mipango ya kiuchumi.
Lakini wataalam wa uchumi wana wasiwasi kuwa huenda uchumi wa China ukazidi kudorola hadi kufikia kiwango cha chini zaidi..BBC
Post a Comment