![]() |
| PICHA MAKTABA |
Na Mwandishi wetu,Mbeya ,Mbeya
Watu 15 wamenusurika kifo baada ya gari
walilokuwa wakisafiria mali ya Kampuni ya
Taqwa Lenye Namba za Usajili T.791 Bzr
aina Ya Nissan Lililokuwa likiendeshwa na Salumu
Selemani (45) Mkazi Wa D’salaam Kuligonga gari namba za usajili T.778
Can Isuzu Ftr likiendeshwa na Edwin
Luyenga (40)
Ajali Hiyo Imetokea Mei 10 mwaka huu Majira ya Saa 2 usiku Katika Kijiji cha Kapyo, Kata ya Mahongole, ,
Wilaya ya Mbarali, Mkoa Wa Mbeya Katika Barabara Kuu Ya Mbeya/Njombe.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa mbeya Nyigesa
Wankyo amewataja baadhi ya majeruhi katika ajali hiyo kuwa ni Apamat Umuyu (41)
Mkongo raia wa nchini Kongo , Salumu Rashidi (29) Mkazi Wa Dsm ,Juma Rajabu (34) Mkazi wa Zanzibar ,Anna Misikita (36) Mkongo , David Mtachi (43) Mkazi Wa Dsm , Groli Amani (41) Mkazi Wa Dsm , Kelvin Jordan (39) Mkazi Wa Dsm.
Majeruhi Wengine ni Lika Ilunga (47) Mkazi Wa Kongo . Majariwa
Ramadhani (51) Mkazi Wa Kagera 12.
Adela Mutomba (46) Mkazi Wa Kongo , Mudy
Abdallah (43) Mkazi Bukoba, Nasoro Mkazi wa Tanga. Ambapo wengine wamekwisha
tibiwa na kupatiwa luhusa katika hospital ya Rufaa Mbeya ambapo chanzo cha hiyo
ni mwendokasi wa dereva wa basi hilo..
Kaimu Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mbeya
Kamishna Msaidizi Wa Polisi Nyigesa Wankyo ametoa Wito Kwa Madereva Kuwa Makini Wanapotumia vyombo
vya moto ikiwa ni pamoja na kufuata sheria za usalama barabarani .
Mwisho.







Post a Comment