Siku 8 zimebaki kufikia kilele cha tuzo za filamu mwaka 2015.
Ikiwa
zimebaki siku chache kufikia kilele cha tuzo za filamu kwa mwaka huu
ambapo Tuzo za Filamu Tanzania (TAFA) zinafanyika kwa mara ya kwanza
nchini Mei 23, 2015 Mwalimu Nyerere International Conference Center
jijini Dar es Salaam.
Haya
ni mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu nchini kwani ni kuonesha
mafanikio. Ni vipengele mbalimbali vilivyopo katika kinyang’anyiro cha
tuzo za filamu mwaka huu 2015. Tuzo hizo ambazo ni kubwa na zenye hadhi
ya juu zimeandaliwa na Shirikisho la Filamu Tanzania na washirika
mbalimbali .
“Kazi
kubwa ya Shirikisho la Filamu Tanzania ni kusaidia kukuza tasnia ya
filamu na kuunga mkono jitihada za wasanii kwa namna mbalimbali. Mbali
na hilo pia ni daraja linalowaunganisha wasanii wa tasnia ya filamu na
Bodi ya Filamu nchini hivyo kurahisisha utendaji wa kazi zao. Ninayo
kamati ya maandalizi iliyo imara na thabiti ambayo imefanya kazi katika
mazingira magumu usiku na mchana kuhakikisha tunapata halfa nzuri na ya
namna yake ambayo haijawahi kutokea”, Alisema Simon Mwakifwamba, Raisi
wa Shirikisho la Filamu Tanzania.
Aliongeza
kwa kusema kuwa tasnia ya filamu nchini bado ina safari ndefu
ukilinganisha na Hollywood ambao wameshapiga hatua kubwa. Tuzo hizi sasa
ni jambo wanapaswa kujivunia kwa wasanii na watengeneza filamu
kujivunia. Imeripotiwa kuwa tasnia ya filamu imechangia kwa kiasi
kikubwa ukuaji wa pato la taifa hili linathibitishwa na taarifa ya
mapato nchini ya hivi karibuni, na hili linadhihirisha kuwa tasnia ya
filamu inafanya kazi kubwa ya kupunguza tatizo la ajira nchini ambalo
limekua ni tatizo kwa vijana wengi hapa nchini.
Mara
baada ya uzinduzi wa tuzo za Filamu mwishoni mwa mwaka 2014
uwasilishwaji wa kazi za filamu ulianza kwa wakati na baadae
zilichaguliwa kwa ustadi mkubwa chache zilizoingia katika kinyang’anyiro
cha tuzo hizi na hatua hiyo ilifanikiwa kikamilifu na baadae kutangaza
washiriki wanaowania tuzo hizi za filamu.







Post a Comment