Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF
iliyoketi jumanne tarehe 5 Mei, 2015 imempiga faini ya sh. 5,000,00 (milioni
tano), Afisa Habari wa klabu ya Yanga SC Jerry Muro kwa kutoa kauli za chuki,
kisirani na uchochezi dhidi ya uongozi wa Bodi ya Ligi (TPLB) nchini na TFF.
Akitoa utetezi wake mbele ya Kamati ya Nidhamu, Jerry Muro
alikiri na kujutia kufanya kosa hilo na kudai ilitokana na ugeni wake katika
uongozi wa michezo, kwa kuzingatia hilo kamati ilimuepusha na adhabu ya
kufungiwa..
Kwa mujibu wa Ibara ya 53 (2)ya Kanuni za Nidhamu za TFF toleo
la 2012, kwa kuidhalilisha TFF na Bodi yake ya Ligi mbele ya umma, kamati
imemtoza faini ya sh. 5,000,000 (millioni tano), Jerry Muro na kuwaonya
viongozi wengine wa familia ya mpira wa miguu kutojihusisha na vitendo vya
matamshi ya aina hiyo.
Shitaka linalomhusisha mchezaji wa Yanga, Amissi Tambwe kumshika
kwa kumdhalilisha mchezaji wa Simba SC Juuko Mursheed, na kiongozi wa Friend
Rangers Hery Chibakasa wa Friends Rangers kuhamasisha vurugu katika mchezo wa
timu yake na dhidi ya Majimaji ya Songea Januari 29, 2015, kamati imeahirisha
mashitaka hayo mpaka tarehe nyingine itakapopangwa.
Kamati iliahirisha malalamiko dhidi ya Mohamed Hussein, Muhibu
Kanu, Manfred Luambano, Venance Joseph, Mussa Senyange, Saleh Ali, Shafii
Maganga na Ismail Salim baada ya kupokea taarifa za udhuru zilizosbabishwa na
mgomo wa madereva wa mabasi ya abiria ya mikoani.
MWISHO.
Post a Comment