Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba
Ushirikiano wa karibu unaozijumuisha Nchi za Jumuiya ya Mataifa ya
Ukanda wa Kusini mwa Bara la Afrika SADC katika masuala ya Ulinzi wa
Anga umesaidia kudhibiti changamoto za Amani na Usalama ndani ya
ukanda huo.
Alisema
uanzishwaji wa Kituo cha pamoja cha uchunguzi wa usalama wa Anga
{ Exercise Blue Okavango } katika Mataifa wanachama wa Jumuiya hiyo ya
SADC umeleta mafanikio makubwa.
Balozi
Seif Ali Iddi alieleza hayo wakati akiufunga Mkutano wa 17 wa siku
mbili wa Wakuu wa Majeshi ya Anga wa Nchi za Kusini mwa Bara la Afrika {
SADC – SAC } uliokuwa ukifanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar
Beach Resort Mzizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Alisema
ndoto iliyobuniwa na Viongozi wa Mtaifa wanachama katika kuanzisha
taasisi hiyo ya ulinzi wa pamoja wa Anga imelenga kuwajengea mazingira
bora ya ustawi wa kuishi kwa amani na utulivu Wananchi wote wa ukanda
wa Sadc.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi wa Kikosi cha Anga cha
Jeshi la Wananchi wa Tanzania kinachoongozwa na Kamanda Mkuu wa Kikosi
hicho Meja Jenerali Joseph Furaha Kapwani kwa kufanikisha vyema Mkutano
huo wa 17 wa SADC – SAC hapa Zanzibar.
Akitoa
shukrani kwa niaba ya washiriki wa Mkutano huo wa 17 wa Sadc – Sac Mkuu
wa Majeshi ya Anga wa Jamuhuri ya Botswana Meja Jenerali Mashinyana
amewashukuru na kuwapongeza Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla kutokana
na ukarimu waliouonyesha.
Kamanda
Mashinyana alisema utulivu walioupata yeye pamoja na Makamanda wenzake
wa Mataifa wanachama wa Sadc – Sac wakati wakiwa Zanzibar umewapa
faraja kubwa watayoendelea kuikumbuka katika maisha yao hata wakati
wameshastaafu kazi ya ulinzi.
Washiriki
wa Mkutano huo wa 17 wa siku mbili wa Wakuu wa Majeshi ya Anga wa Nchi
za Kusini mwa Bara la Afrika { SADC – SAC } pia walipata fursa ya
kutembelea sehemu mbali mbali za Kihistoria pamoja na maeneo ya matunda
na Viungo.CREDIT MICHUZI
Post a Comment