Na Baraka Kizuguto,Dar es salaam
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) leo inashuka dimbani
kucheza mchezo wake wa pili dhidi ya timu ya Taifa kutoka Madagascar, mchezo
utakaochezwa katika uwanja wa Royal Bafokeng majira ya saa 12 jioni kwa saa za
Afrika Mashariki.
Taifa Stars inahitaji kupata ushindi katika mchezo wa leo dhidi
ya Madagascar ili kufufua matumaini ya kuweza kusonga mbele katika hatua
inayofua ya Robo Fainali.
Kocha
Mkuu wa Taifa Stars akiongelea mchezo wa leo amesema, makosa yaliyojitokeza
katika mchezo dhidi ya Swaziland yamefanyiwa kazi na anaamini vijana wake
watafanya vizuri.
“Mchezo
wa Swaziland tulipata nafasi nzuri za kufunga, lakini washambuliaji wangu
hawakuwa makini kuzitumia nafasi hizo, tatizo la kupoteza nafasi nyingi
limefanyiwa kazi na nina amini leo vijana watafanya vizuri” alisema Nooij.
Aidha
Nooij amesema anataarajia mchezo kuwa mgumu kutokana na Madagascar kuhitaji
ushindi wa pili mfululizo, baada ya kuifunga Lesotho katika mchezo wa awali,
Nooij ameahidi kufanya vizuri katika mchezo huo.
Mchezo
huo utakuwa moja kwa moja (Live) katika kituo cha Superspot SS4, na SS9.
Naye
kiungo wa Taifa Stars, Said Juma Makapu anarejea nyumbani leo usiku kwa usafiri
wa Shirika la ndege la Fastjet kwa ajili ya kufanyia vipimo zaidi na matibabu,
anatarajiwa kuondoka uwanja wa O.R. Tambo saa 5 usiku kufika uwanja wa JK
Nyerer saa 8 usiku.
Mwisho.






Post a Comment