![]() |
| Taarifa hiyo iliyotolewa bungeni imesema Hyon Yong-Chol alipigwa na kombora la kuangusha ndege mbele ya mamia ya maafisa wakuu serikalini |
Idara ya ujasusi ya Korea Kusini
imesema kuwa waziri wa ulinzi wa Korea Kaskazini ameuawa kwa kutokuwa
muaminifu kwa kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong-un.
Taarifa hiyo
iliyotolewa bungeni imesema Hyon Yong-Chol alikutana na mauti yake baada
ya kupigwa kwa kombora la kuangusha ndege mbele ya mamia ya maafisa
wakuu serikalini mwishoni mwa mwezi Aprili.
Bwana Hyon anasemekana
kuwa alisinzia katika hafla iliyokuwa ikihutubiwa na rais Kim jambo
lililomuudhi sana kiongozi huyo wa kiimla.
Hata hivyo ukweli wa ripoti hiyo haujabainika kutokana na usiri wa serikali ya Korea Kaskazini.
Bwana Hyon alipandishwa cheo
na kuwa Generali mwaka wa 2010 na kuuawa kwake kunatia shaka udhabiti wa
uongozi wa rai Kim Jong -un.
Hyon alipandishwa cheo na kutangazwa kuwa waziri wa usalama wa taifa mwaka uliopita.
Mwandishi
wa BBC aliyeko huko Seoul anasema mauaji hayo ya kikatili mbele ya umma
ikiwa yatathibitishwa, yanaonyesha athari za uasi dhidi ya Kim
Jong-un.
Mapema idara hiyo ya ujasusi ilisema viongozi wakuu katika serikali ya Korea Kaskazini wamekuwa wakiuawa kila mmoja kwa wiki.
Mara ya mwisho kwa kiongozi huyo wa korea kaskazini kuamrisha kuuawa
kwa kiongozi mkuu serikalini ilikuwa ni mwaka wa 2013 alipoamrisha ami
wake
Chang Song-thaek - kukamatwa na kutiwa kitanzi.
Chang alikamatwa katika mkutano wa hadhara na kupelekwa katika eneo la hadhara alikouawa mbele ya umma.BBC SWAHILI







Post a Comment