Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kama wewe ni moja ya watu wanaomfuatilia kwenye mtandao picha wa Instagram, utakuwa umejionea ni kwa kiasi gani staa mrembo wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper anapenda MITINDO.
Akizungumza na mtandao wa bongo 5, ambao ulitaka kujua mapenzi yake  kwenye fashion na kama anapata changamoto kuhakikisha anapendeza muda wote.

 “Ni hobby sana sana, hakuna challenge kwasababu kila mtu anapenda kitu chake,” amesema Wolper. “Mimi napenda kuvaa.”
Katika hatua nyingine Wolper amesema ameshafikiria kuja na kipindi cha TV cha masuala ya fashion lakini anahitaji kujifunza zaidi.
“Movie ni kazi yangu ambacho ni kipaji changu lakini hivyo vingine nina idea navyo kidogo tu na kuna watu ambao tayari wameshaingia kwahiyo vitu vingine mpaka nijifunze labda ndio niingie.”
Wolper pia alisema bado amesimama kufanya filamu kutokana na sababu mbalimbali za kwenye tasnia  hiyo  japokuwa amekili kuwa kuwakosesha vitu mashabiki wake kwa kipingi hiki ila watajua ila watakuja kujua tu  sababu ya yeye kusimama.
Bongo 5

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top