![]() |
| Mshindi wa gari akiwa katika gari lake |
![]() |
| Mshindi katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa masoko utafiti na huduma kwa wateja Bi.Tully Mwambapa pamoja na baadhi ya maofisa wa benki ya CRDB Tawi la Mwanjlewa jijini Mbeya |
![]() |
| Mkurugenzi wa masoko utafiti na huduma kwa wateja Bi.Tully Mwambapa akizungumza katika hafla hiyo. |
Benki ya CRDB leo imekabidhi zawadi ya gari aina ya Passo mshindi wa shindano la tuma pesa na simbanking shinda passo kwa mfanyabiashara kutoka Zanzibar ambaye
hufanya biashara zake jijini mbeya Ndugu Mwinyi Hamisi ikiwa ni gari ya pili kutolewa toka kuanza
kwa shindano hilo.
Akikabidhi gari hilo kwa niaba ya
Mkurugenzi Mkuu, Dk. Charles Kimei, katika hafla fupi iliyo fanyika katika
benki CRDB Tawi la Mwanjelwa Mkurugenzi Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja,
Tully Mwambapa, amesema promosheni hiyo ni moja ya mikakati iliyojiwekea Benki ya CRDB katika kuhakikisha inaongeza chachu na kukuza uchumi kwa wateja wao .
.
Amesema kupitia huduma
ya SIMBANK mteja anaweza kushinda zawaidi hiyo ya gari
kwa kutuma pesa au kutoa pesa kupitia huduma ya simu ambapo moja kwa moja
ataingizwa katika promosheni hiyo .
Kutokana na shindano hilo amesema
kuwa vijana wanapaswa kuachana
na matumizi mabaya ya simu ambayo
yamekuwa yakiwaingiza katika maovu na hivyo waitumie huduma
hiyo kwa ajili ya kuwawezesha
kupata huduma bora na
ya haraka yenye usalama mkubwa
sanjali na kupata zawadi nyingi.
Amesema,
wanatambua changamoto zilizopo ndani ya jamii na kwamba serikali pekee haiwezi
kuzitatua, hivyo wao kupitia huduma za
kibenki wameamua kuanzisha shindano hilo
ili kuwapa motisha zaidi wateja wao.
Aidha, Sherehe hiyo iliyoenda
sanjari na sherehe za siku ya Mtoto wa Afrika , wafanyakazi wa benki hiyo
walitumia fursa hiyo kuburudika na watoto zaidi ya 50 walioletwa na wazazi wao
kwa ajili ya kuwafungulia akaunti ya Jumbo Junior.
Akizungumzia akaunti hiyo maalumu
kwa watoto Mkurugenzi huyo wa masoko alisema akaunti hiyo ni nguzo kubwa kwa
maendeleo ya watoto,
kwani kupitia akaunti hiyo wazazi wanaweza
kuwa na uhakika wa kutimiza malengo ya kielemu kwa watoto wao
Naye mshindi huyo baada ya kukabidhiwa funguo ya gari hilo lenye thamani ya shilingi Milioni 12, alisema amefurahi sana kwa kushinda zawadi ya gari kutoka CRDB kwani imembadilishia mfumo wa maisha yake.
Aidha ametoa wito kwa jamii kuacha
tabia ya kumiliki simu kubwa pasipo kuwa na malengo ya aina yeyote badala yake
watumie kujifunza mambo mbalimbali hususani katika suala la kufahamu
masoko na namna ya kupanua biashara
zao.
Mwisho















Post a Comment