| Wanachama wakimsikiliza Makongoro |
MTOTO
wa muasisi wa Taifa la Tanzania, Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius
Kambarange Nyerere, Makongoro Nyerere, amesema amewataka watanzania kuumpa ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama
cha mapinduzi ccm ili aweze kurudisha heshima ya chama hicho katika uchaguzi
mkuu ujao mwezi octoba .
Makongoro,
amesema hayo , wakati wa zoezi la kuwapata wadhamini watakao mdhamini nafasi ya
urais ambapo katika zoezi hilo zaidi ya mamia ya wanachama wa Chama Cha
Mapinduzi CCM, na wakazi wengine wa Mkoa wa Mbeya, jana Jumatatu Juni 8,
2015, walifurika kwa wingi kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya,na kumdhamini
kiongozi huyo.
Akizungumza
na umati huo mkubwa katika ukumbi wa ccm
jijini mbeya , Makongoro aliwataka wakazi wa Mkoa wa Mbeya kuhakikisha
wanamuunga mkono wa kumchagua kuwa rais na kuachana na wagombea ambao
wameonekana kutokuwa watiifu na waadilifu kwa chama na Taifa kwa
ujumla hali ambayo imechangia kwa kiwango kikubwa chama hicho kupoteza mvuto
wako .
Aidha,
Makongoro amesema kuwa chama cha mapinduzi kimekuwa kikiongozwa
na taratibu zake ambazo zinapaswa kufuata na wananchama wote.
Amesema
waasisi wa chama hicho ambao ni hayati baba wa Taifa Mwalimu Julias nyerere
walikiacha chama hicho katika mstari mzuri hali ambayo kwa sasa imekuwa tofauti
hivyo kuna haja ya kufanya mabadiliko
kwa kuhakikisha hali hiyo inalejea kama kawaida.
Mwisho.






Post a Comment