| Afisa Mahusiano Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira jijini Mbeya (Uwsa)Neema Stantony |
Na Mwandishi wetu,Mbeya
Mamlaka Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Mbeya (UWSA)imeamua kuboresha mfumo wa huduma za ulipaji wa ankara za maji kwa wateja wake kwa kutumia huduma za M-pesa,Tigo Pesa pamoja na mitandao mingine ikiwa na lengo la kuongeza idadi ya walipaji wa huduma hiyo sanjali na kuondoa adha kwa wateja wao.
Akizungumza jijini
Mbeya Afisa mahusiano Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira (Uwsa) Ndugu
Neema Stantony amesema mfumo wa ulipaji wa huduma za maji kupitia mitandao hiyo
ya simu umeleta urahisi wa malipo ya
huduma ya maji mahala popote pale
nchini.
Amesema hatua hiyo mpya imechangia kwa kiasi kikubwa
kuleta huduma bora kwa wakazi wa mji wa Mbeya katika viwango vya juu zaidi.
Amesema mara badaa ya kaunzisha huduma hiyo mwitiko umekuwa mkubwa sana hasa kutokana na kupungua kwa foleni wakati
wa ulipaji wa Ankara hizo sanjali na kuwepo kwa ongezko kubwa la watu kulipa Ankara
zao.
Amesema mfumo huo
umeondoa usumbufu wa kutumia muda mrefu
kwenye foleni za kulipia huduma ya maji nakwamba huduma hiyo ni
hatua ya kipekee hasa ikizingatiwa kuwa badala ya kupoteza muda kukaa foleni
mteja anaweza kuendelea na shughuli zake za kila siku.
Aidha Neema
amesema changamoto kubwa iliyopo kwa sasa ni kwa baadhi ya wateja kulipa Ankara
zao za maji katika mamlaka nyingine za
maji kama Dawsco hivyo kuletea usumbufu wakati wa ufuatiliaji.
Amesema hali hiyo
pia inatokana na baadhi yao kusahau
akaunti zao sanjali na kutokuwa makini
wakati wa ulipaji wa huduma hiyo.
Wakati huo huo
Afisa huyo amewaondoa hofu nwakazi wa jiji la mbeya ambao wanapata huduma ya
maji kwa muda mfupi kuwa suala hilo linatokana na kuhalibiwa kwa miundombinu ya
maji hasa kwa maeneo ambayo kunafanyika matengenezo ya barabara.JAMIIMOJABLOG
Mwisho.






Post a Comment