Viongozi wa Umoja wa Ulaya
wakiendelea na kikao chao hadi usiku wa manane mjini Brussels
wamekubaliana kuwahamisha maelfu ya wahamiaji ambao waliingia katika
nchi za Italia na Ugiriki.
Mwenyekiti wa kikao hicho Donald Tusk
amesema wahamiaji 40,000 watapelekwa katika mataifa mengine ya Ulaya
katika kipindi cha miaka miwili ijayo.
Hata hivyo, hakutakuwa na mgawanyo wa lazima kwa nchi kuwapokea wahamiaji hao.
Mgogoro
wa madeni ya Ugiriki pia ulizungumziwa katika kikao hicho. Ugiriki na
wakopeshaji wake wa kimataifa bado hawajafikia muafaka baada ya
mazungumzo ya Alhamisi.
Mapema, Bwana Tusk amezitaka nchi wnachama wa EU kugawana mzigo wa wahamiaji haram ambao wamevuka bahari ya Mediterani.
Takwimu
mpya kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR
zinaonyesha wahamiaji 63,000 waliingia Ugiriki kwa njia ya bahari mwaka
huu na wengine 62,000 waliingia nchini Italia. Viongozi hao pia
wamekubali kuwapokea wakimbizi wengine 20,000 kutoka nje ya Umoja wa
Ulaya.
Uingereza imejitoa katika mpango huo, ambapo mataifa ya
Ulaya mashariki yamekataa kukubaliana na kugawana wahamiaji, kwa hiyo
itabaki kuwa hiyari. Hatua ya nchi hizo imemwuudhi Waziri Mkuu wa Italia
Matteo Renzi, ambaye amesema mpango huo ni mzuri.
Italia imeomba msaada zaidi kutoka washirika wake wa EU kushughulikia mzigo wa wahamiaji.BBC SWAHILI







Post a Comment