Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Na Frank Shija, WHVUM 
Bodi ya Filamu Tanzania imepongeza kwa juhudi zake za kuendeleza na kusaidia kukua kwa tasnia ya filamu nchini. Pongezi hizo zimetolewa juzi jijini Dar es Salaam na Balozi Paul Rupia alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Filamu ya Desire to Succeed. 
Balozi Rupia alisema kuwa tasnia ya filamu inazid kukua nchini sambamba na kuongezeka kwa wasanii kuzingatia maadili ya Kitanzania. 
"Niseme wazi tu kwamba Serikali kupitia Bodi ya Filamu nchini inafanya kazi thabiti tofauti na ilivyokuwa huko nyuma ambapo watendaji wa Bodi hiyo walikuwa na kazi ya kukagua tu tofauti na sasa wanatoka na kuhamasisha ukuaji wa tasnia hii” Alisema Balozi Rupia. 
Aidha Balozi Rupia ametoa rai kwa taasisi za umma na binafsi kutambua mchango wa wasanii na kuwatumia vyema katika program zao za kujitangaza ndani na nje ya nchi kama ambayvo DCB benki ilivyotumia fursa hiyo. 
Kwa upande wake Mwakilishi wa Kampuni ya Consnet Group Bw. Sanctus Mtsimbe amesema kuwa imekuwa ni faraja kwa wasanii kuona kuwa kazi zao na mchango wao katika jamii unatambuliwa na baadhi ya taasisi hapa nchini na kuongeza kuwa hiyo inaonyesha dalili njema katika ukuaji wa tasnia ya filamu. 
Aliongeza kuwa katika filamu ya hiyo ya Desire to Succeed wasanii wameitendea haki kazi yao na kwa kuzingatia matakwa ya kanuni na maelekezo ya Bodi ya Filamu Tanzania ikiwa ni pamoja na kuzingatia mavazi yenye staha kwa mujibu wa maadili ya kitanzania. 
Mtsimbe ametoa rai kwa wadau wa tasnia ya filamu kununua nakala za filamu hiyo ambayo itapatikana madukani kwa bei ya shilingi 3000/= ili wajionee namna kazi nzuri ya wasinii wetu. Filamu ya Desire to Suicceed ni filamu ya kwanza nchini Tanzania ambayo maudhui yake yamekuwa na malengo makuu mawili kwa wakati mmoja ikiwa ni kuelimisha na matangazo ya biashara kwa wahusika kutumia Bidhaa za Benki ya DCB katika kuuisha hadithi yao. DCB Benki ndiyo mdhamini wa filamu hiyo ambaoyo imetengenezwa na Kapmuni ya Consnet Group huku ikishirikishwa wasanii Tito Mrisho Zimbwe (Muhusika Mkuu), Rose Ndauka,Jackline Pentezel, Hidaya Njiadi, Gojak na wengine.
Kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo, msanii Rose Ndauka, Tito Mrisho Zimbwe na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashara ya DCB Balozi Paul Rupia wakionyesha DVD ya filamu ya Desire to Succeed juzi jijini Dar es Salaam mara baada ya kuzinduliwa rasmi. Filamu hiyo imetengezwa na kampuni ya Consnet Group chini ya udhamini wa DCB Benki ikiwa ni njia ya kujitangaza kupitia ubunifu wa sanaa ya filamu.
Picha na Frank Shija, WHVUM:

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top