| WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akizungumza na wanachama wa ccm mkoa wa mbeya ambao walijitkeza kwa lengo la kumdhamini. |
Heka heka na kuelekea katika uchaguzi mkuu mwezi octoba
umezidi kupamba moto ambapo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) makada mbalimbali
waliotangaza nia ya kuwania nafasi ya urais kupitia chama hicho wameendelea na
mchakato wa kutafuta wadhimi katika mikoa 15 ya Tanzania bara na Zanzibar katika kutekeleza taratibu zilizowekwa na
chama hicho.
Hadi sasa katika mkoa wa mbeya makada watatu wamekwisha kamilisha zoezi hilo
la kutafuta wadhamini ambao ni Waziri wa Uchukuzi Samwel Sitta ,Mtoto wa
hayati mwalimu nyerere Makongoro pamoja
na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikinao wa kimataifa Bernard Membe ambapo kila mmoja alitumia
nafasi hiyo kujinadi na kumwaga sera zake .
Hii leo June 10 WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe, amesema endapo Kamati kuu
ya CCM haitalipitisha jina lake katika kuwania nafasi ya kuteuliwa kugombea
nafasi ya urais kwa mwaka 2015, kura yake ataipeleka kwa mgombea Marck
Mwondosya.
Amesema, miongoni mwa wagombea wote waliotangaza nia
yakuwania kuteuliwa kugombea nafasi ya urais kupitia chama cha mapinduzi CCM ni
wagombea wawili tu akiwemo yeye na Mark
Mwandosya ambao wameweza kukidhi vigezo vya kuliongoza Taifa hili.
Akizungumza, wakati wa zoezi la
kuwapata wadhamini watakao mdhamini nafasi ya urais ambapo katika zoezi hilo
zaidi ya mamia ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM, na wakazi wengine wa
Mkoa wa Mbeya, walifurika kwa wingi kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya,na
kumdhamini kiongozi huyo.
Amesema, kama asipo pitishwa yeye yupo tayari
kukaa chini kumpisha Mwandosya kwani ni kiongozi shupavu na muadilifu na
amejaliwa kuwa na kila dhamana ya kuliongoza Taifa la Tanzania.
Aidha, Membe aliwataka wakazi wa
Mkoa wa Mbeya, kuhakikisha wanayapitisha majina mawili ya wagombea wa nafasi za
urais likiwemo jina lake na la Mark Mwondosya.
Mwisho.






Post a Comment