Alisema filamu nyingi zina picha zisizofaa kwa watoto hivyo zionyeshwe usiku wa manane ambapo inaaminika kwamba muda huo idadi kubwa ya watoto huwa wamelala.
Naye memeja mkuu wa kampuni hiyo, Omari Zuberi, alisema kampuni hiyo imewekeza dola milioni moja kwa kipindi cha miaka 10 ili kusaidia Tamasha la Filamu Zanzibar (ZIFF) kupata watu wenye vipaji ndani na nje ya nchi.
Katika tamasha hilo, filamu zitakazoshindandishwa katika kipengele cha ‘Zuku Bongo Movies’ ni Mapenzi ya Mungu,Mr.Kadamanja, Fundi Seremala, Daddy’s Wedding, VIP, Single Zero,Kutakapokucha,Msago, Mikono Salama na Nyange Kigoma.
Nyingine ni Mbawa Mwitu, Samaki Mchangani,Faraja, Pichu, Going Bongo na Kilimo 2.
Hata hivyo mkurugenzi wa Tamasha hilo, Prof.Martin Mhando alisema kwa pamoja ZIFF na Zuku wanasaidia kuendeleza tasnia yafilamu za bongo kwa kuwa wanathamini sanaa ndiyo maana wanaamini kwamba itasaidia kuwaongezea ujuzi watayarishaji wa filamu zakiswahili kwa kuwa hitaji la filamu zao ni kubwa.
Mtanzania
Post a Comment