Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi


Mbeya

Watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wavamia na kujeruhi na kisha kupora mali mbalimbali baada ya kuweka kizuizi cha mawe na magogo katika barabara ya mbalizi-mkwajuni.



Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa 02:00 huko eneo la msitu wa mlima msangamwelu, kijiji cha mjele, kata ya mshewe, , wilaya ya mbeya vijijini, mkoa wa mbeya.



Aidha katika tukio hilo wahanga hao ambao walikuwa wanakwenda galula kuhudhuria sherehe ya upadrisho, waliporwa pesa taslimu ambazo bado kufahamika kiasi gani, mabegi ya nguo mbalimbali, zawadi za waumini,  simu za mikononi pamoja na majoho.  Wahanga wamepatiwa matibabu na kuruhusiwa.





Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ndugu Ahmed Msangi amesema  kuwa   watu hao ambao majina yao hayakufahamika mara moja ambao wanasadikiwa   kuwa majambazi walitumia mbinu ya  kuliwekea vizuizi gari lenye namba za usajili Sm 3496 aina ya toyota land cruiser mali ya hospitali ya mwambani chunya lililokuwa likiendeshwa na dereva loved mwandongo (53) mkazi wa mkwajuni.



Aidha gari hiyo  hiyo ilikuwa imebeba mapadri watatu  wanafunzi ambao ni ambao ni  Furaha Henjewele (36)Mkazi wa Mbeya alipigwa fimbo kichwani na kukatwa panga mkono wa kulia.



Wengine ni pamoja na  Padri Gasper Mwashimwanga (37) mkazi wa mpuguso – tukuyu  Henry Mwalyanga (33) Eliakim kasegila (27)  mkazi wa peramiho  na  Padri bonifasi chalo (46) mkazi wa mwanjelwa.



Msako mkali unaendelea ili kuwabaini waliohusika katika tukio hili ili wakamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao
mwisho

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top