Rais
mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi akisisitiza jambo wakati akifungua
Maonyesho ya 5 ya Sayansi kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini
katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. (Picha zote na
Daniel Mbega wa www.brotherdanny.com).
Mkurugenzi
Mtendaji wa Young Scientists Tanzania (YST) Dk. Gosbert Kamugisha
akimtambulisha Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kwa Balozi wa Kenya nchini
Tanzania Chirau Ali Mwakwere kabla ya kufungua maonyesho hayo mwishoni
mwa wiki.
Na Daniel Mbega wa brotherdanny.com
RAIS
mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, amewataka walimu
katika shule za msingi na sekondari kutumia lugha ya Kiswahili
kufundisha sayansi, kwani lugha hiyo inaeleweka vizuri.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho ya Tano ya Sayansi kwa wanafunzi
wa shule za sekondari nchini jijini Dar es Salaam jana, Alhaj Mwinyi
amesema Kiswahilini lugha inayoeleweka vizuri, si kwa wanafunzi tu,bali
hata kwa watu wengine, hivyo ni vyema walimu wakaweka mkazo katika
kuitumia kwenye masomo ya sayansi.
“Nimepita
kwenye maonyesho haya, baadhi ya wanafunzi walikuwa wananiuliza
‘tukueleze kwa Kiswahili au kwa Kiingereza’, nikasema tumieni lugha
yoyote tu. Wengine wamenieleza Kiingereza na wengine Kiswahili.
Balozi
wa Kenya nchini, Chirau AliMwakwere (wa pili kushoto) na Balozi wa
Ireland nchini, Fionnuala Gilsenan wakisikiliza kwa makini maelezo ya
wanafunzi walioshiriki maonyesho hayo. Nyumaya Balozi Gilsenan ni Dk.
Gosbert Kamugisha, Mkurugenzi Mtendaji wa Young Scientists Tanzania.
Mgeni
rasmi katika ufunguzi wa maonyesho hayo, Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi
(katikati) akifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa wakati
wa utuaji wa tuzo. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
wa YST, Prof. Eligius Lyamuya. Wengine ni Balozi wa Ireland nchini,
Fionnuala Gilsenan na Balozi wa Kenya nchini, Chirau Ali Mwakwere.
“Lakini
nataka niwaambie, walionieleza kwa Kiswahili, pamoja na utafiti wao
kuwa katika lugha ya Kiingereza, walifafanua vizuri sana na nikasema
‘aah, kumbe Kiswahili kinaweza kutumika kufundisha vizuri sayansi,”
alisema.
Aliongeza
kusema kwamba, yeye wakati anaingia darasa la tano, mwalimu wake wa
sayansi alikuwa rais wa Scotland, lakini alimfundisha sayansi kwa
Kiswahilina ndio msingi wake mkubwa wa kulifahamu vyema somo la sayansi.
Akizungumzia
maonyesho hayo yaliyoandaliwa na kuratibiwa na taasisi ya Young
Scientists Tanzania (YST), Alhaj Mwinyi amesema ni jitihada nzuri za
kuandaa wataalam wa kesho katika sayansi.
Maonyesho
hayo yalifanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee yakishirikisha jumla
ya wanafunzi 240na walimu 120 kutoka shule 120 nchini.
“Hii
inafurahisha kuona watoto wadogo wanaichambua sayansi kwa kufanya
tafiti hizi nzuri kabisa na kwa hakika nawapongeza sana waandaaji na
muendelee hivyo hivyo kuandaa kizazi cha sayansi,” alisema Alhaj Mwinyi.
Wadhamini
wakuu wa maonyesho hayo, Kampuni ya BG Tanzania, wamesema wataendelea
kudhamini maonyesho yajayo ili kuweka hazina ya wataalamu wa sayansi wa
kesho.
“Sisi
tunajihusisha na utafiti wa gesi na mafuta, tunahitaji wanasayansi
wataalamu ambao lazima tuanze kuwekeza sasa, ndiyo maana katika
maonyesho ya mwaka huu tumetoa Dola 200,000 na mwakani tutatoa kiasi
kingine ambacho kinaweza kuwa kama hicho au zaidi,” alisema Makamu Rais
wa BG Tanzania, John Ulanga, ambaye anayeshughulikia Sera na Masuala ya
Uhusiano.
Naye
Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Fionnuala Gilsenan, ambao ni
wadhamini wa maonyesho hayo, alisema nchi yake itaendelea kuunga mkono
jitihada za YST kama ambavyo wamekuwa wakifanya tangu maonyesho hayo
yalipoanza mwaka 2011.
Katika
maonyesho hayo ya tano, wanafunzi wa Mzumbe Sekondari kutoka Morogoro,
Edwin Luguku na John Method, ndio walioibuka washindi wa jumla kutokana
na utafiti wao usemao “Kupunguza Matumizi ya Mifuko ya Plastiki
Tanzania” (Reducing The Use of Plastic Bags in Tanzania).
Kwa
ushindi huo, vijana hao ambao mbali ya kupata medali na tuzo na
wamepata zawadi ya hundi ya Shs. 1 milioni. Walikabidhiwa zawadi zao na
Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
Washindi
wa pili walikuwa Emmanuel Lemalali na Emmanuel Sanga kutoka Tanga
Technical na utafiti wao wa ‘A Simple Method For Controlling
Ecto-parasites’, ambao wamepata medali na tuzo pamoja na hundi ya Shs. 1
milioni, ambapo walikabidhiwa zawadi zao na Balozi wa Ireland nchini,
Fionnuala Gilsenan.
Zawadi
nyingine kwa washiriki wa maonyesho hayo zilikuwa katika makundi manne
ambayo ni Sayansi ya Baolojia na Ikolojia (Biological and Ecological
Sciences) iliyodhaminiwa na Taasisi ya Afya Ifaraka; Sayansi ya
Kemikali, Hisabati na Fizikia (Chemical, Mathematical and Physical
Sciences) iliyodhaminiwa na Taasisi ya Fizikia (Institute of Physics);
Sayansi ya Kijamii na Kitabia (Social and Behavioural Sciences)
iliyodhaminiwa na shirika la Concern; na Teknolojia (Technology)
iliyodhaminiwa na Karimjee Jivanjee Foundation.
Katika
makundi hayo, mbali ya kupatiwa medali na tuzo, washindi wa kwanza
walipata Shs. 500,000, washindi wa pili Shs. 300,000 na washindi wa tatu
Shs. 200,000.
Aidha,
wadhamini wengine wa maonyesho hayo walitoa zawadi mbalimbali ambao ni
Songas, Read International, Solaris, Spicenet, Karimjee Jivanjee,
Masumin Printways, First Car Rental, Vernier, na Human Development
Innovation Fund (HDIF).
Washindi wa tuzo maalum:
Tuzo ya Kupenda Sayansi ya Songas: Venance Msechu na Martin Oisso kutoka St. Jude Sekondari, Arusha na utafiti wao ‘Automatic House Control System’.
Tuzo ya Read International: Evance
Marumbwe na Sara Ismail kutoka Mtapika Sekondari, Mtwara na andiko lao
la ‘Mbinu za Ufundishaji Zinachochea Kukua kwa Taaluma (Do Teaching
Methods Influence Academic Performance?)
Tuzo ya Solaris: Emmanuel Lemalali na Emmanuel Sanga kutoka Tanga Technical na utafiti wao wa ‘A Simple Method For Controlling Ecto-parasites’.
Tuzo ya Masumin Printways: Maregesi Nyamajeje na Peter Kailembo kutoka Mwasele Sekondari, Shinyanga na andiko lao la ‘Designing a Temperature Sensor’.
Tuzo ya First Car Rental: Augustino
Simon na Felister Stanley kutoka Butimba Day, Mwanza na utafiti wao wa
Who Votes In Mwanza? (Nani Anayepiga Kura Mwanza?).
Tuzo ya Vernier: Tunu Ngajilo na Ally Salum kutoka Mbeya Sekondari na utafiti wao wa Automatic Irrigation System.
Tuzo ya HDIF: Tunu Ngajilo na Ally Salum kutoka Mbeya Sekondari na utafiti wao wa Automatic Irrigation System.
Tuzo ya Spicenet: Geofrey
Ndunguru na Yusuph Mwenda, Songea Boys, na utafiti wao wa Analysis of
Blind Students Attitude Towards Science (Uchambuzi wa Hulka ya Wanafunzi
Wasioona Katika Mwelekeo wa Sayansi).
Washindi wa makundi mbalimbali:
Sayansi ya Baolojia na Ikolojia:
1. Mariam Ngaula na Latifa Mussa kutoka Kilakala Sekondari, Morogoro na utafiti wao wa ‘The Scarcity of Water in Morogoro’.
2. Saada Abeid na Zaina Maliki wa Mtwara Girls na utafiti wao wa ‘Leaching effects for Maize growing In Mtwara’.
3.
Latifa Hamad Ali na Salma Hussein Haji kutoka Kiembe Samaki Sekondari,
Zanzibar na utafiti wao wa ‘Exploring Lippia Asperifolia Leaves
(Mpambaake) On Anaemic Pregnant Women’.
Sayansi ya Kemikali, Hisabati na Fizikia:
1. Adil Abdallah na Kevin James kutoka Loyola Sekondari, Dar es Salaam na utafiti wao wa ‘Micro Plastics In Drinking Water’.
2.
Maryam Salim na Betty Pentzel kutoka Popatlal Sekondari, Tanga na
utafiti wao wa ‘The Effects Of Chemical Hair Products And Its Solution’.
3. Patrick Boniface na Jacob John kutoka Mara Sekondari na utafiti wao wa ‘First Principle Of Integration’.
Sayansi ya Kijamii na Kitabia:
1.
Latifa Mohamed na Raphael F. Nyamhanga wa Mtwara Technical na utafiti
wao wa ‘Is ICT the solution to poor academic performance?’
2.
Nancy George na Christermine Christopher kutoka Debrabant Sekondari,
Dar es Salaam na utafiti wao wa How To Reduce Road Accidents In Kilwa
Road (Jinsi ya Kupunguza Ajali za Barabarani Katika Barabara ya Kilwa).
3.
Aloyce Botto na Devis Mafuru wa Tumbi Sekondari, Kibahana utafiti wao
wa ‘Swahili Language As A Medium For Learning And Instructions In
Tanzania’.
Teknolojia:
1. Venance Msechu na Martin Oisso kutoka St. Jude Sekondari, Arusha na utafiti wao ‘Automatic House Control System’.
2. Tunu Ngajilo na Ally Salum kutoka Mbeya Sekondari na utafiti wao wa Automatic Irrigation System.
3.
Salivius Simon na Derick Deusdedit kutoka St. Joseph Kolping Sekondari
na utafiti wao wa ‘Carrying Capacity Governing Device’.
Tuzo ya Karimjee Jivanjee:
Washindi
ambao watafadhiliwa masomo ya shahada ya kwanza chuo kikuu ni Petro
Samson Ndegeleki na Juma Joshua Wiliam kutoka Nassa Sekondari ambao
utafiti wao ulihusu ‘How Different Natural Fertilizers Affect the Growth
Of Maize’. Washindi hao pia watagharamiwa safari ya kwenda Dublin,
Ireland kuhudhuria maonyesho ya sayansi ya BT YSTE Januari 2016.
Washindi wa Pili wa jumla:
Emmanuel Lemalali na Emmanuel Sanga kutoka Tanga Technical na utafiti wao wa ‘A Simple Method For Controlling Ecto-parasites’.
Washindi wa Jumla 2015:
Edwin Luguku na John Method wa Mzumbe Sekondari na andiko lao la ‘Reducing the use of plastic bags in Tanzania’.
(Imeandaliwa na www.brotherdanny.com)
Brother Danny Blog (Kisima cha Hekima na Busara)
Cell: +255 - 715 - 070 109
Whatsapp: +255 - 656 - 331 974
Post a Comment