Dirisha
la Usajili kwa wachezaji wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Ligi Daraja la kwanza
(FDL), na Ligi Daraja la Pili (SDL) linatarajiwa kufungwa kesho Alhamis saa
sita usiku.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini (TFF), linavikumbusha vilabu vyote vinavyoshirki msimu
mpya wa 2015/2015 kuhakikisha vinakamilisha usajili wa wachezaji wao kabla ya
dirisha la usajili kufungwa kesho.
Kipindi
cha dirisha la usajili kwa timu za Ligi Kuu, Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la
Pili kilifunguliwa Juni 15, 2015 na kitamalizika kesho kwa awamu ya kwanza ya
usajili.
TWIGA STARS KUINGIA KAMBINI
KESHO ZANZIBAR
Timu
ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) inatarajiwa kuingia kambini
kesho kisiwani Zanzibar kujiandaa na Fainali za Michezo ya Afrika (All Africa
Games) zitakazofayika mwezi Septemba mwaka huu nchini Congo Brazzavile.
Kikosi
hicho cha wachezaji 25 chini ya Kocha Mkuu Rogasian Kaijage, tayari kimeanza
mazoezi kujiandaa na michuano hiyo ambapo Tanzania ilikata tiketi ya kushiriki
fainali hizo baada ya kuiondoa Zambia kwa jumla ya mabao 6-5.
Twiga
Stars inaingia kambini kwa gharama za
TFF, huku jitihada za TFF kuwasiliana na Kamati ya Olimpiki nchini (TOC)
zikiendelea kuona ni jinsi gani kamati hiyo inaihudumia timu hiyo ya Taifa kwa
ajili ya maandalizi ya michuano hiyo ya Michezo Afrika.
TFF
inatambua TOC ndio wana jukumu la kuhudumia timu za Taifa kuelekea kwenye
michuano hiyo ya Michezo ya Afrika ikiwemo Twiga Stars.
Twiga
Stars ambayo imefuzu kwa Fainali za Michezo ya Afrika itakayoanza kutimua vumbi
Septemba 04 – 17 imepangwa kundi A na wenyeji Congo Brazaville na Nigeria
pamoja na Ivory Coast.
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Post a Comment