Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 Muungano wa wasanii wameandaa hafla maalum ya kumshukuru na kumuaga Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na kumpongeza na kumkaribisha Mheshimiwa John Pombe Magufuli ,Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi,inayofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City .

 Mgombea wa Urais kupitia CCM  Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye ukumbi wa Mlimani City tayari kuhudhuria  hafla maalum ya kumshukuru na kumuaga Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na kumpongeza na kumkaribisha Mheshimiwa John Pombe Magufuli.wengine pichani ni Ruge Mutahaba ,Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye .
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Paul Makonda.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akisalimina na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mhe. January Makamba
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwa kwenye picha ya pamoja na msanii Diamond ,Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul Makonda na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mhe. January Makamba.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top