Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za
pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Burundi (FBF) Reverien
Ndikuriyo kwa kuchaguliwa kuwa spika wa bunge la Seneta nchini humo.
Katika
salam hizo za pongezi kwa Rais wa FBF na nakala zake kwenda CECAFA, CAF na
FIFA, Malinzi ameelezea imani yake kwa Seneta Ndikuriyo na amemtakia kila la
kheri na mafanikio katika nafasi hiyo mpya aliyochaguliwa.
TWIGA STARS YAENDELEA
KUJIFUA ZANZIBAR
Kikosi
cha timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) kilichoweka kambi kisiwani
Zanzibar, kujiandaa na fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) kimeendelea
kujifua kutwa mara mbili katika viwanja wa Aman na Fuoni kabla ya safari ya
kuelekea nchini Congo – Brazzavile mwezi ujao.
Twiga
Stars chini ya kocha mkuu Rogasian Kaijage inatarajiwa kucheza mchezo wa
kirafiki na timu ya Taifa ya Kenya (Harambee Starlets) Agosti 23 katika uwanja wa Amani kisiwani Zanzibari
ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michezo ya hiyo ya Afrika (All Africa Games).
Kaijage
amesema anashukru vijana wake wanafanya mazoezi kwa morali ya hali ya juu,
wachezaji wanaonekana kuyashika vizuri mafunzo yake na kumpa imani kuwa sasa
kikosi chake kimeiva na anachosubiri ni mchezo wa kirafiki dhidi ya Kenya ili
kuweza kuona uwezo wa kikosi chake kabla ya safari ya kuelekea nchini
Congo-Brazzavile.
Akiongeleaa
maendeleo ya kambi ya Twiga Stars, Mkuu wa Msafara Blassy Kiondo amesema timu
ipo katika hali nzuri, wachezaji wanafanya mazoezi kwa morali ya hali ya juu, hakuna majeruhi
kikubwa wanachosubiri kwa sasa ni huo mchezo wa kirafiki dhidi ya Kenya
mwishoni mwa wiki ijayo.
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Post a Comment