Mamlaka nchini Indonessia inasema
kuwa ndege moja ya abiria iliowabeba watu 54 wakiwemo watoto watano
imepoteza mawasiliano na idara ya kituo cha udhibiti safari za ndege.
Maafisa
wa idara ya uchukuzi wanasema kuwa ndege hiyo inayomilikiwa na huduma
ya Trigana Air ililikuwa ikielekea katika mji wa Oksibil
mashambani,mashariki mwa jimbo la Papua kabla ya kutoweka.
Msemaji wa wizara hiyo amesema kuwa hatua za kuisaka ndege hiyo
zimeanza na zinashirikisha mamlaka ya eneo hilo na kwamba hali mbaya ya
hewa katika milima ya eneo hilo inaathiri harakati hizo.
Waandishi
wanasema kuwa taifa la Indonesia lina rekodi mbaya ya ajali za ndege
huku ajali mbili zikiwa tayari zimeripotiwa mwaka mmoja ulioipitaNdege ya Indonesia Air ilianguka katika bahari ya Java mwezi Disemba
ilipokuwa ikitoka Sura Baya kuelekea Singapore na hivyobasi kuwaua watu
wote 192 walioabiri chombo hicho.
Vilevile ndege moja ya kijeshi
ilianguka katika makaazi ya watu huko Medan Sumatra mnamo mwezi Julai na
kuwaua zaidi ya watu 140 ikiwemo watu kadhaa ardhini.
Post a Comment