Ratiba
ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara (VPL) imetoka leo ambapo jumla ya
timu 16 zinashiriki ligi hiyo itakayoanza kutimua vumbi Septemba 12
katika viwanja tofauti nchini na kumalizika Mei 7, 2016.
TFF
inavisisitiza vilabu kukamilisha usajili wao wa wachezaji na viongozi
kabla ya kufungwa kwa dirisha hilo la usjaili kesho alhamisi Agosti 20,
2015. Baada ya kufungwa kwa usajili huo hakutakua na muda tena wa
nyongeza.
Kwa
klabu ambayo haitawasilisha malipo ya ada ya mchezaji wa kigeni ya dola
elfu mbili (U$D 2000) mchezaji huyo hataruhusiwa kucheza kwenye ligi
hadi malipo hayo yatakapofanyika.
Michezo
saba itachezwa siku ya ufunguzi jumamosi katika viwanja tofauti ambapo
Ndanda Vs Mgambo Shooting (Nang’wanda - Mtwara), African Sports Vs Simba
SC (Mkwakwani - Tanga), Majimaji Vs JKT Ruvu (Majimaji - Songea), Azam
FC Vs Tanzania (Azam Complex - Dsm), Stand United Vs Mtibwa Sugar
(Kambarage - Shinyanga), Toto Africans Vs Mwadui (CCM Kirumba - Mwanza),
na siku ya jumapili Young Africans Vs Coastal Union (Taifa – Dar es
salaam).
Post a Comment