Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatarajia kumpeleka katika kamati ya
maadili ya TFF Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya DRFA Ndg. Rashid
Saadallah siku ya Alhamisi tarehe 27/08/2015 saa 9:00 alasili kwa kosa
la kudharahu na kupingana na maagizo ya mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi
ya TFF.
Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi ya TFF alimwagiza asimamishe
uchaguzi wa chama cha mpira wa wilaya ya Temeke (TEFA), ili kuitisha
fomu zote za waomba uongozi pamoja na maamuzi ya kamati za TEFA na DRFA
ili kujiridhisha kama taratibu zilifuatwa katika mchakato huo kutokana
na malalamiko ya baadhi ya wagombea kwamba hawakutendewa haki.Pamoja na kupata barua hiyo kutoka kwa mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya TFF aliandika barua ya kukataa kutii maagizo hayo. TFF imechukua hatua hiyo kulinda nidhamu kwa vyombo vilivyo chini ya TFF.
Post a Comment