Kamati ya Uchaguz ya TFF imeyaomba majalada hayo ili ijiridhishe na kuona haki inatendeka kwa wagombea wote na baadae tarehe mpya ya uchaguzi itatolewa.
SAANYA KUCHEZESHA AZAM Vs YANGA
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limemteua mwamuzi wa kati Martin Saanya kuchezesha mchezo wa Ngao ya Jamii jumamosi, badala ya mwamuzi Israle Nkongo aliyekua amepangwa awali.
Mwamuzi Israel Nkongo anasumbuliwa na matatizo ya misuli ya paja, ambayo itampelekea kukaa nje ya uwanja kwa takribani siku kumi, hali iliyopeleka TFF kumbadilisha mwamuzi huyo kuelekea kwenye mchezo huo wa jumamosi
Post a Comment