Wafuasi wa rais Yoweri Museveni
wamewashambulia wafuasi wa Amama Mbabazi nyumbani kwake katika kitongoji
kimoja cha mji mkuu wa Kampala.
Vijana hao waliokuwa wamevalia
shati zenye maandiko ya kumuunga mkono rais Museveni walishambulia boma
la kiongozi huyo ambaye ameahidi kuwania kiti cha urais dhidi ya rais
Museveni katika uchaguzi mkuu ujao.Vijana hao walimtuhumu waziri huyo mkuu wa zamani kwa kuwapa ahadi hewa kuwa angewapa kazi.
Wafuasi wa Mbabazi walipopata habari nao wakakimbia kumuokoa na hapo ndipo makabiliano baina yao yakatokea.
Jarida la Daily Monitor linasema kuwa wafuasi hao wa Mbabazi waliwapura kwa mawe na vijiti.
Rais Museveni alikuwa mwandani
wa karibu sana wa mpinzani wake Mbabazi katika chama tawala cha NRM na
hata Mbabazi alihudumu kwa miaka mingi kama kiongozi mkuu chamani.
Hata hivyo uhusiano baina ya wawili hao uliharibika Mbabazi alipofutwa kazi kama waziri mkuu na akatangaza kuwa angempinga rais Museveni katika uchaguzi mkuu ujao.
Wachanganuzi wa maswala ya siasa nchini Uganda wanasema kuwa japo rais Museveni amekuwa akishindana na wapinzani katika chaguzi zilizopita,kuingia uwanjani kwa waziri mkuu wa zamani Amama Mbabazi ndio changamoto kubwa kwa utawala wa Museveni.

Post a Comment