Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Mizengo Peter Pinda(katikati) akipokea Salaam kutoka
kwa Gwaride lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la
Kwanza kwa Askari wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani). Kushoto ni
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(kulia) ni Mkuu wa Chuo
cha Magereza Kiwira, SACP. Stanford Ntirundura.
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Peter
Pinda akikagua Gwaride rasmi lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya
Uongozi wa Daraja la kwanza akiongozwa na Kamanda wa Gwaride. Sherehe
hizo zimefanyika leo Agosti 15, 2015 katika Chuo cha Magereza Kiwira,
Mbeya.
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Peter
Pinda akitoa cheti cha sifa kwa Mwanafunzi Mhitimu wa Mafunzo hayo, Wdr.
Raymond Mgosso ambaye amefanya vizuri masomo ya Darasani(kushoto) ni
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja.
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Peter
Pinda akiwa jukwaani akifuatilia kwa makini Onesho Maalum la zoezi la
kujihami(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja.
Gwaride la Wahitimu wa Mafunzo ya
Uongozi Daraja la kwanza likipita mbele ya Jukwaa kutoa heshima kwa
Mgeni rasmi kwa mwendo wa haraka.
Askari wa Kike ambao wamehitimu Mafunzo hayo wakionesha zoezi la kujihami(Self Defence).
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini hafla ya kufunga Mafunzo hayo ya Uongozi.
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Peter
Pinda akiongozana na Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa
pili kushoto) kuelekea kwenye Ukumbi wa Chuo cha Magereza Kiwira kwenye
hafla ya kufunga Mafunzo hayo(wa kwanza kushoto) ni Katibu Mkuu Wizara
ya Mambo ya ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil.
Mgeni rasmi Waziri Mkuu Mhe.
Mizengo Peter Pinda akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wa Mafunzo
ya Uongozi Daraja la Kwanza(wa pili kulia) ni Katibu Mkuu Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil(wa tatu kulia) ni
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa tatu kushoto) ni
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro(wa kwanza kulia) ni Kamishna Mkuu
wa Idara ya Uhamiaji, Sylivester Ambokile(wa kwanza kushoto) ni Kamishna
wa Utawala na Fedha, Gaston Sanga(wa pili kushoto) ni Mkuu wa Chuo cha
Magereza Kiwira, SACP. Stanford Ntirundura.
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza)
Post a Comment