Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akizungumza katika sherehe hizo za wakulima Nanenaneb Kanda ya Nyanda za juu kusini katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya. |
Waandishi wa habari wakiwa kazini |
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikabidhi zawadi kwa washindi wa manesho hayo katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya Agost 8 mwaka huu. |
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipotembelea baadhi ya mabanda ya waoneshaji katika sherehe hizo za wakulima Nanenane . |
Burudani. |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema mchakato wa
kumpata mgombea wa urais kupitia chama
cha mapinduzi (CCM) umekwenda vizuri hivyo
kwa wale wale ambao hawakufikia malengo nivema wakakubali matokeo kwani ilikuwa lazima mmoja apatikane.
Amesema busara nzuri ni kukubali matokeo hayo badala ya
kuhama chama kama walivyo fanya baadhi ya makada wengine wa chama hicho.
Waziri Mkuu Pinda ametoa kauli hiyo mkoani
mbeya wakati akifunga maadhimisho ya sherehe za wakulima Nanenane kwa mikoa ya kanda za nyanda
za juu kusini katika viwanja vya John Mwakangale.
Amesema, katika mchakato wa
kuomba nafasi ya urais wagombea walikuwa zaidi ya 40 lakini aliyekuwa
akihitajika mmoja hivyo ni vema wengine ambao majina yao yaliondolewa kutokana
na kutokidhi vigezo mbalimbali vya chama wangekubali matokeo kuliko
kuhama chama.
Amesema yeye kwa upande wake ameridhika na
mchakato huo hivyo haoni sababu ya kuondoka
ndani chama hicho kwani ndicho chama kilicho mfikisha hapo alipofikia sasa nakutumikia
nafasi hiyo ya uwaziri Mkuu kwa miaka 8 hadi anakoma utumishi wake.
Pinda amesema kama kuna mambo ya kusahishana atafanya
hivyo akiwa ndani ya chama cha mapinduzi kwani hata huko ambako wengine wamehamia hakuko
salama na kunachangamoto nyingi hiyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi
kupiga kura na kumchagua kiongozi bora atakaye wafikisha mahala pazuri.
Hata hivyo, aliwataka wanachama wa
CCM kutambua kuwa sera nzuri za vyma ndizo zitakazo saidia kuwashawishi
watu kukikubali chama hivyo hakuna sababu ya kuhama zaidi ni kuziboresha sera
zilizopo ili watu wazipende na kuzikubali
Katika hotuba yake waziri Mkuu Pinda
amewataka viongoizi wa mikoa hiyo ya kanda za nyanda za juu kusini kuhakikisha wanajikita katika kuwasaidia
wakulima na wafugaji wadogo wadogo ili kuwainua kiuchumi badala ya kushughulika
na wakulima wakubwa pekee.
Amesema uchumi wa Tanzania unakuwa lakini
bado hauendani na hali hali ya maisha ya watanzania hivyo kuna kila sababu ya
kuendelea kupigana na hali ya umasikini
sanjali na kuondoa utofauti ya
aliye nacho na asiye nacho.
Hata hivyo waziri Mkuu Pinda
amesema anajivunia katika kipindi cha utumishi ndani ya serikali ya rais
kikwete kwa kuweza kuinua sekta ya
kilimo kwani
nchi imeweza kupeleka tanni 500 za mahindi katika nchi jirani ya Ethiopia,
Sudani tanni 500, Burundi tanni 500 , Malawi tanni 500 na nchi nyingine za
jirani hivyo hii ni hatua kubwa sana .
Mwisho.
Post a Comment