Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli pamoja na mgombea ubunge wa jimbo la Same Mashariki Mama Anne Kilango wakiwasalimu wakazi wa Same waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni za CCM Ndungu.PICHA NA MICHUZI JR-KILIMANJARO.
  Wakazi wa Same Mashariki wakimsikiliza Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli.
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli akimvalisha fulana mmoja wa wafuasi wa CHADEMA alieamua kurejea chama cha CCM jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni ndani ya jimbo la Same Mashariki
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Ndungu kweye mkutano wa kampeni Same Mashariki,jioni ya leo.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwa sambamba na Mgombea Ubunge wa jimbo la Vunjo,Innocent Shirima wakiwapungia wananchi walipokuwa wakiwasili kwenye mkutano wa kampeni mjini himo.
 Wakazi wa Himo wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli.
  Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge jimbo la Vunjo kupitia CCM Innocent Shirima.
  Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Mwanga Profesa Jumanne Maghembe kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika Mwanga.
 
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Same Magharibi kwenye uwanja wa Kwasakwasa ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa katika uongozi wake atahakikisha kodi ndogo ndogo zinaondolewa kwa wafanyabiashara wadogo.
 wakazi wa Same Magharibi wakishangilia mara baada ya kumsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwenye uwanja wa Kwasakwasa ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa katika uongozi wake atahakikisha kodi ndogo ndogo zinaondolewa kwa wafanyabiashara wadogo.
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Ndugu Augustino Lyatonga Mrema mara baada ya kukutana njia panda ya Himo.
 Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Ndugu Augustino Lyatonga Mrema akizungumza mbele ya mgombea wa urais kupitia CCM na kuwataka wananchi wa Vunjo kumpigia kura mgombea wa urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli kwani ni rafiki wa kweli kwa maendeleo ya Tanzania.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top