Kwa mara nyingine jeshi la anga la Israel lashambulia Ukanda wa Gaza Jumatatu kwa madai kuwa wanachama wa Hamas walivurumisha makombora dhidi ya İsrael.Jeshi la Israel lilifahamisha kuwa wapiganaji wa Hamas walirusha kombora kutokea Ukanda wa Gaza na kuangukia Kusini mwa Israel bila ya kusababisha hasara.
Msemaji wa jeshi la Israel, Peter Lerner alifahamisha kuwa makombora 18 walirushwa kutokea Gaza kuelekea Israel tangu mwanzoni mwa mwaka 2015.
Ifahamike kuwa zaidi ya wapalestina 2,100 waliuawa na wengine zaidi ya 11,000 kujeruhiwa katika operesheni ilioendeshwa kwa muda wa sik 51 Julai mwaka 2014 na jeshi la Israel.
Mashambulizi hayo yaliharibu nyumba 17,200, miskiti 73 na shule 24 Ukanda wa Gaza.CHANZO TRT SWAHILI
Post a Comment