Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Na Mwandishi Wetu
Msanii Nguli wa filamu nchini, Ray Kigosi, amewaambia watanzania leokuwa makini na kusikiliza sera na kuachana na mihemko ya kisiasa itakayopelekea wao kufanya maamuzi watakayoyajutia baadae.

Kigosi ameyasema hayo alipokuwa katika moja ya mikutano inayoendeshwa na kundi la wasanii lenye kauli mbiu ya Nimestuka, katika jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya ziara ya kundi hilo inayopita kijiji kwa kijiji katika kuhakikisha kwamba wanawaelimisha vijana wenzao kuhusiana na usikilizwaji wa sera na mapokeo ya demokrasia kwa jamii.
Awali akiongea kabla ya kuwakaribisha wenzake 12 alioandamana nao, Kigosi amesema yeye alipokuwa Ukawa alikuwa akishuhudia vijana wakihamasishwa kupinga hata mambo yanayoonekana kuwa na tija yaliyofanywa na seriikali jambo ambalo yeye mwenyewe aliliona kuwa ni upotoshwaji wa wazi wazi.
"Naamini kuwa mpinzani, sio kupinga kila kitu, walipaswa pia kutufundisha jinsi ya kukabiliana na maisha kama vijana, lakini nikaja kugundua nimekosea sana kuacha kuungana mkono na Magufuli", alikiri Kigosi.
PICHANI JUU: Msanii wa filamu Ndende, akihamasisha wananchi wa Kishapu  kuhusiana na kumuunga mkono mgombea wa Chama cha Mapinduzi, Dk John Pombe Magufuli
Mchekeshaji Kitale, akiongea katika Mkutano wa Kampeni ya Nimes'tuka, inayoendeshwa na wasasnii wa filamu na muziki wa kizazi kipya, uliofanyika katika jimbo la Kishapu jioni hii
Inspekta Haroun, mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya akitoa burudani kwa wakazi wa jimbo la Kishapu baada ya mkutano wao wa kampeni ya Nimes'tuka, inayoendeshwa na wasanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, wanaokiunga mkono Chama cha Mapinduzi
Muigiza filamu maarufu, Kajala Masanja, akiongea katika mkutano wa kampeni za Nimes'tuka, uliofanyika katika jimbo la Kishapu mchana wa leo, kulia ni Ray Kigosi
Mchekeshaji Mboto, naye ni mmoja kati ya wasanii wanaoendesha kampeni za Nimes'tuka, hapa akiongea na wananchi wa jimbo la Kishapu, mkoani Shinyanga
Muigizaji Skyner Ally naye akimwaga sera zake katika kampeni za Nimes'tuka
Miss Tanzania 2014, Lilian Kamanzima, akiongea na wananchi wa jimbo la Kishapu jioni ya leo katika mkutano wa kampeni za Nimes'tuka
Mikono juu...
Ray Kigosi akimwaga sera...
Msanii wa vichhekesho, StanBakora naye akiongea yake Kishapu leo

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top