Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi |
Na
Jamiimojablog
Jeshi la
Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia watu 274 kwa tuhuma za kuhusika na vitendo vya vurugu
wakati wa utangazaji wa matokeo ya uchaguzi katika majimbo matatu yaliyopo
Mkoani hapa.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake ,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed
Msangi,alisema watuhumiwa hao tayari wamefikishwa katika mahakama za mwanzo
zilizomo katika Wilaya husika.
Msangi, ameyataja
majimbo hayo ni Rungwe, jimbo la Mbozi pamoja na jimbo la Vywawa ambapo maeneo
hayo yalionekana kuwepo na viashiria vya wagombea kutokubaliana na matokeo
hivyo wafuasi wao kuchukua uamuzi wa kuvunja sheria kwa kuanzisha vurugu.
Amesema,vurugu
hizo ziliambatana na uharibifu mkubwa wa mali za umma ikiwemo miundombinu ya
barabara.
Aidha,
Kamanda Msangi amesema kuwa mbali na uharibifu huo pia vurugu hizo zilisababisha
kutokea hali ya uvunjifu wa amani iliyochangia kwa kiasi kikubwa kuwatia hofu
baadhi ya wananchi ambao ni wapenda amani.
Hata
hivyo, Msangi alisema atuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani leo kwa makosa
tofauti tofauti.
Mwisho.
Post a Comment