Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa michuano ya Kombe la
Shirikisho (AzamHD Federation Cup) utakaofanyika leo Jumatatu, saa 9
kamili mchana katika uwanja wa Karume ambapo timu ya Abajalo FC itacheza
dhidi ya Transit Camp zote za jijini Dar es salaam.
Michuano hiyo ilianza kutimua vumbi jana kwa mchezo mmoja kuchezwa
katika uwanja wa Karume uliopo mjini Musoma, ambapo Vill Squad ya jijini
Dar es salaam iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 3- 1 dhidi ya timu ya
JKT Rwamkoma ya mkoani Kagera.
Katika uwanja wa CCM Kirumba, Pamba FC ya jijini humo watakua wenyeji
wa timu ya wachimba dhahabu kutoka mkoani Shinyanga, Bulyanhulu FC
mchezo utakaoza saa 10:30 jioni.
Jumla ya timu 64 zinashiriki michuano hiyo kutoka Ligi Kuu, Ligi
Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kuwania kutwaa ubingwa, ambapo
Bingwa wa michuano AzamHD Federation Cup atapata nafasi ya kuwakilisha
nchi kwenye Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka 2017.
Post a Comment