Inasadikika watu kadhaa wamepoteza Maisha na wengine wamejeruhiwa leo baada ya basi la New Force kupata ajali Eneo la Mahenge Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa barabara kuu ya Iringa- Dar es salaam
Basi hilo lilikuwa likitokea mkoani Mbeya kuelekea Dar es Salaam ambapo lilipata ajali mchana huu jitihada za kuondoa miili na kusafirisha majeruhi kupeleka hospitali zinaendelea, Bado kamanda wa polisi mkoani Iringa Kamanda Peter Kakamba anatafutwa ili kuthibitisha tukio hilo na kuelezea idadi ya waliofariki na majeruhi katika ajali hiyo.
Post a Comment