Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Kisukari ni ugonjwa wa kongosho, wakati uzarishaji wa Insulini au utolewaji wake haufanyi kazi vizuri, na ikiwa hali hii haitadhibitiwa, inaweza kusababisha matatizo makubwa kwenye macho, figo, neva, mishipa ya damu, Ini na moyo.
Kuna aina kuu mbili za kisukari:
• Kisukari aina ya kwanza, ambapo Insulini inakuwa tegemezi (insulin-dependent); hapa kongosho halitengenezi kabisa insulini au linaitengeneza kwa kiasi kidogo sana kiasi kwamba mgonjwa analazimika kuchomwa sindano ya insulini au kutumia pampu za insulini.
• Kisukari aina ya pili ni wakati ambapo insulini inakuwa huru (insulin-independent) au inapatikana lakini kongosho haliitoi na hivyo dawa (kemikali) lazima itumike kulilazimisha kongosho kutoa insulini.
Aina ya kwanza ya kisukari inaweza kutokea kwa watu kuanzia utotoni mpaka kwa watu wa umri wa miaka 30. Aina hii ya kisukari hushambulia kwa haraka sana, kwa kawaida ndani ya majuma mpaka miezi kadhaa. Kwakuwa kongosho halifanyi kazi vizuri, usawa wa damu sukari lazima upewe uangalizi wa karibu. Watu wenye kisukari aina hii ya kwanza pia huwa na uzito pungufu (underweight).
Aina ya pili ya kisukari huanza kujitokeza kuanzia umri wa miaka 40 na kinachosababisha ni miaka mingi ya kula chakula kisicho sahihi, kutofanya mazoezi au sababu za kurithi (genetics). Kwa bahati mbaya, nyakati hizi tunashuhudia hata watoto wadogo wakipatwa na aina hii ya kisukari. Watu wenye kisukari cha aina hii ya pili pia huwa na uzito uliozidi (overweight).
Baadhi ya dalili kuu za kisukari ni:
• kiu iliyozidi
• kukojoa mara kwa mara
• kupatwa na ganzi kwenye miguu na mikono
• kujisikia mchovu
• kutoona vizuri
• kuongezeka njaa
• kushindwa kuhimili tendo la ndoa.
Ikiwa daktari atakuona una dalili za kuwa na kisukari, ata kutaka ufanye jaribio la kuiandaa glukozi katika usawa wake wa chini kabisa kwenye damu (fasting plasma glucose test – fpgt), kwa sababu hiyo, atakutaka ubaki bila kula kitu chochote kwa muda usiopungua masaa nane kabla ya kukupima, ambapo kwa kawaida huwa ni asubuhi ili kupata uwezekano wa damu sukari kuwa katika usawa wake wa chini kabisa.
Kisha atachukua damu toka kwenye mkono na kuipima na kulinganisha matokeo na uwiano ufuatao:
• Chini ya 99 mg/dl ni kawaida
• 100 – 125 mg/dl ni hatua za mwanzo za kisukari
• Zaidi ya 126 mg/dl ni kisukari.
Kisukari ambacho hakikudhibitiwa kinaweza kusababisha mwili kulazimika kuanza kuchoma mafuta ili kuzarisha nishati (diabetic ketoacidosis), hii kwa kawaida hutokea kwa watu wenye kisukari cha aina ya kwanza ambapo glukozi inaweza kuingia kwenye seli bila insulini.
Kitendo cha mafuta kutumika kuzarisha nishati huzarisha taka nyingi za asidi zilijulikanazo kwa kitaalamu kama ‘Ketones’.
Taka hizi (Diabetic ketoacidosis – DKA) hujijenga kwenye mzunguko wa damu na kusababisha pumzi fupi, mauzauza na kutapika na mwishowe kukuwekea koma na hata kusababisha kifo.
DKA haijitokezi sana siku hizi ahsante kwa insulini na vifaa rahisi kutumia kufuatilia damu sukari.
Wakati damu sukari inapokuwa nyingi na damu inapokuwa imetulia, nene na hafifu (hyperosmolar syndrome), husababisha kukojoa mara nyingi ili kuilazimisha sukari iliyozidi kutoka nje. Ikitokea hivyo, utapatwa na upungufu mkubwa wa maji na unaweza kushikwa na mikakamao ya miguu, mapigo ya moyo kwenda mbio, mauzauza, msukosuko, au hata kuelekea kwenye koma. Hii huwatokea watu wenye kisukari aina ya pili ambao hawafuatilii kujuwa kiasi cha damu sukari yao mwilini.
Moja kati ya matatizo makubwa ya kisukari ni kitendo cha kushuka kwa kiasi kikubwa cha damu sukari mwilini (hypoglycemia), hii hutokea wakati damu sukari inazarishwa kidogo kutokana na kutumia kiasi kingi cha insulini au kukaa muda mrefu bila kula chochote na huku ukiwa umetumia insulini au ulinusa harufu ya chakula fulani.
Zifuatazo ni dalili za kushuka kwa damu sukari mwilini:
• Kichwa kuuma
• Mauzauza
• Mapigo ya moyo kwenda mbio
• Kutokwa na jasho jingi
• Kuona vitu viwili katika kimoja.
Ikiwa damu sukari itashuka kufikia usawa wa 50 – 70 mg/dl, unaweza kujisikia kuwa na hali zifuatazo:
• Kuishiwa nguvu
• Kusinzia na kizunguzungu
• Kuona nukta nukta kabla ya macho yako
• Mwili unaweza kuwa kama uliopooza.
Wakati damu sukari imeshuka kufikia 30 – 45 mg/dl, unaweza kwenda kwenye koma (deep sleep) na kufa ikiwa hautapewa sukari ya haraka kama inayopatikana kwenye juisi ya chungwa (huitwa muokoaji kwenye uwanja wa madawa), sukari halisi au peremende ya sukari ili kupandisha kiwango cha damu sukari mwilini.
Namna moja ambayo kisukari kinaweza kujipenyeza taratibu kwenye miili ya watu, ni pale insulini inapofanya ukaidi bila wao kujua, ukaidi huu wa insulini ukitokea, kuna uwezekano mkubwa wa wewe kupatwa na kisukari wakati fulani katika safari yako ya kuishi.
Ukaidi wa insulini (insulin resistance) ni wakati ambapo mwili unazarisha insulini lakini hauitumii ipasavyo.
Insulini ni homoni inayotengenezwa na kongosho ili kuusaidia mwili kuitumia glukozi kwa ajili ya kuzarisha nishati. Glukozi ni aina ya sukari ambayo ni chanzo kikuu cha nishati ya mwili.
Mfumo wa umeng’enyaji wa chakula, hukimeng’enya chakula na kuwa glukozi ambayo kisha husafiri kwenye mkondo wa damu mwili mzima. Glukozi inapokuwa kwenye damu huitwa damu glukozi, pia hujulikana kama damu sukari. Wakati damu sukari inapopanda juu baada ya kula, kongosho huitoa insulini ili kuziwezesha seli za mwili wako kuitumia glukozi.
Mtu anapokuwa katika hali ya ukaidi wa insulini, mishipa, mafuta na Ini lake vinakuwa haviitiki vema kwa insulini, kwa sababu hii, mwili wake utaihitaji insulini zaidi ili kuiwezesha glukozi kuziingia seli.
Kongosho litajaribu kukidhi ongezeko la uhitaji huo wa insulini kwa kuizarisha insulini nyingi zaidi. Hatimaye kongosho halitaweza kuendelea kumudu kuzarisha kiasi hicho kingi cha insulini. Insulini na Glukozi iliyozidi, vitajijenga ndani ya mkondo wa damu vikiandaa ngazi kuelekea kisukari.
Katika kitabu cha dr.Batman, ‘your bodies many cries for water’ anasema ikiwa mwili una kiasi kidogo cha maji na chumvi, ubongo utakuwa unajiendesha kwa karibu ya aslilimia 100 kwa kutumia sukari.
Ubongo pia utapandisha juu kiwango cha sukari kwenye damu ili kuuwezesha kufanya kazi zake vizuri. Cha kushangaza ni kuwa, mwili unaihitaji insulini ili kuuwezesha kuitumia sukari kama chanzo cha nishati, lakini kamwe ubongo hauihitaji insulini ili kuupelekea mahitaji yake ya nishati.
Katika kisukari, ubongo unajipa moyo wenyewe kama vile daktari ampavyo moyo muathirika wa kisukari kwa kutumia dripu zenye sukari na chumvi (intravenous fluid treatment).
Watu wengi wenye kisukari huwa hawaelewi ni kwanini wanakuwa na damu sukari nyingi wakati waamkapo asubuhi ikiwa hawakula kitu chochote kabla ya kwenda kulala. Sababu ni kuwa, usiku unapokuwa umelala, mwili hufanya kazi kwa bidii kujiripea wenyewe, katika kufanya hivyo, mwili hutumia sukari. kwakuwa haukula chochote kabla ya kwenda kulala, mwili lazima ujile wenyewe (cannibalize off itself) ili kuliwezesha Ini kutengeneza sukari kwa ajili ya nishati.
Ubongo, ambao ni kituo kikuu cha udhibiti wa kazi zote za mwili, utagunduwa kuwa hakuna kiasi cha kutosha cha sukari kwenye damu kwa ajili ya matumizi yake, na kwa sababu hiyo utaliamuru ini kutoa mara mbili mpaka tatu ya kiasi cha sukari ikiwa damu itaihitaji. Hii ndiyo sababu ya kupanda kwa kiwango cha sukari asubuhi kama hukula chochote kabla ya kwenda kulala.
Inashauriwa kwa watu wenye kisukari kula gramu 25 mpaka 30 za maharage machanga ya kijani kibichi au njegere (green beans), siagi halisi na chumvi dakika 15 kabla ya kwenda kulala, hii itasaidia kushusha damu sukari waamkapo asubuhi. Maharage haya yana kiasi kidogo cha wanga (carbs), na kiasi kingi cha protini, magnesiamu na asidi amino iitwayo ‘tryptophan’ ili kuubeba mwili usiku mzima.
Katika kuepuka sukari, baadhi ya watu wenye kisukari huamua kutumia viongeza sukari visivyo vya asili (artificial sweeteners). Viongeza utamu hivi visivyo vya asili pia huongezwa katika soda na juisi nyingi za viwandani. Unapoweka sukari ya kutengenezwa ulimini au unapokunywa kinywaji au kula chakula kilichoongezwa sukari za kutengenezwa, ulimi utauambia ubongo kuwa sukari inakaribia kuja, ubongo utaliambia Ini liache kuendelea kutengeneza sukari bali liihifadhi kwa ajili ya matumizi ya baadaye na lijiandae kuishughurikia sukari iliyopo njiani kuja. Muda wote ini huwa bize likitengeneza sukari mwilini.
Ubongo upo makini sana (very smart), baada ya muda yaani baada ya hiyo sukari ya kutengenezwa kutua chini tumboni utagundua kuwa hakuna sukari iliyoliwa bali ulilaghaiwa au ulidanganywa. Dakika hii mzunguko wa damu unakuwa katika udharura wa uhitaji wa sukari.
Fikiri: Kila siku unaenda dukani kununua unga wa ugali kilo moja. Siku moja unafika dukani mwenye duka anakuambia unga umebaki kilo tatu na hajuwi lini atapata mzigo mwingine. Utafanya nini?. Utafanya kila uwezalo uzichukuwe hizo kilo tatu zilizopo kama tahadhari kesho usishinde bila kula.
Ndicho kinachotokea mwilini. Ubongo ukishagunduwa kuwa iliyoliwa haikuwa sukari na ulishaliamuru Ini kupumzika kuitengeneza sukari kwenye mzunguko, utaliamuru Ini kuipatia damu mara mbili mpaka tatu ya kiasi cha sukari zaidi ya inavyohitajika!. Sasa unapoenda kupima kiasi cha damu sukari, unajikuta huelewi nini cha kufanya kwa sababu kipo juu mno. Na sasa lazima uchomwe insulini ili kuishusha damu sukari.
Dr.Batman, anasema; ‘kwa sehemu kubwa, kisukari ni matokeo ya kukosa maji, chumvi, magnesiamu, asidi amino (tryptophan) ipatikanayo kwenye mayai, maharage, vyakula jamii ya karanga na jibini, vitamini B6, zinki na mazoezi’.
Unapokuwa katika upungufu wa maji (haunywi ya kutosha) na unakula vyakula vyenye chumvi kidogo au visivyo na chumvi kabisa, ‘automatikali’ ubongo utapandisha kiwango cha sukari kwenye damu yako.
DAWA MBADALA 10 ZINAZOTIBU KISUKARI
Je kisukari kinatibika? Ndiyo kisukari kinatibika. Mhimu ni upate tiba mbadala au tiba asilia ambazo ni sahihi.
Umakini unahitajika sana hasa kwa mgonjwa yule ambaye ameanza kutumia dawa za hospitalini kila siku. Nakushauri usianze kuzitumia hizi dawa moja kwa moja ukiwa peke yako bila uangalizi wa karibu wa daktari au mganga wa tiba za asili.
Twende sasa tuzichambuwe hizi dawa moja baada ya nyingine kama ifuatavyo;
Dawa mbadala 10 zinazotibu Kisukari
1. UWATU
Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa uwatu unao uwezo mkubwa katika kutibu kisukari. Uwatu huzisisimua seli katika kongosho kitendo kinachofanya uzalishwaji wa insulini kuongezeka. Maajabu haya ya uwatu yanasemekana kufanyika kutokana na uwatu kuwa na asidi amino mhimu sana ijulikanayo kama ‘4-hydroxyisoleucine’. Miaka mingi kabla hata ya huu utafiti kufanyika, uwatu umekuwa ukitumika kama moja ya dawa bora kabisa za asili katika kutibu kisukari.
Namna ya kuutumia Uwatu kujitibu kisukari
• Chota mbegu za uwatu vijiko 4 na uziloweke katika maji robo lita kwa usiku mmoja. Asubuhi ponda ponda hizo mbegu za uwatu ndani ya maji kisha zichuje na upate maji yake. Kunywa maji haya kila siku asubuhi kwa muda wa miezi 2.
• Chukuwa uwatu ya unga vijiko vikubwa 2 na uweke ndani ya maziwa au maji ya uvugu uvugu robo lita, koroga vizuri na unywe kila siku kutwa mara 2 kwa miezi 2.
• Chukuwa gramu 100 za mbegu za uwatu na gramu 50 za binzari manjano. Unaweza kuongeza kiasi kidogo cha pilipili manga nyeupe kwenye mchanganyiko huu. Ongeza kijiko 1 cha mchanganyiko huu wote katika maziwa robo lita na unywe kutwa mara 2 kila siku.
• Unaweza pia kuongeza uwatu ya unga katika unga wako unaotumia kutengenezea mkate au hata chapati.
2. MDALASINI
Utafiti uliofanywa kwa watu wenye kisukari aina ya pili umeonyesha kuwa utumiaji wa gramu 1 hadi 6 za mdalasini kwa siku unaweza siyo tu kupunguza kaisi cha damu sukari mwilini, bali pia unaweza kupunguza kiasi cha mafuta mazito katika damu (triglyceride) na hata kudhibiti kolesto!
Waathirika wa kisukari pia hutokewa kuwa na matatizo katika mfumo wao wa upumuwaji, hivyo utumiaji wa mdalasini kwao unaleta maana zaidi kwakuwa mdalasini unao uwezo mkubwa katika kuzuia magonjwa katika mfumo wa upumuwaji pia.
Mdalasini ya unga hushusha kiwango cha damu sukari kwa kuziamsha shughuli za insulini. Mdalasini pia ina faida kwa watu waliogunduliwa kuwa na kisukari cha mwanzo (pre-diabetes status) na hivyo matumizi ya mdalasini kwao yatasaidia kuzuia wasipatwe na kisukari katika siku za usoni.
Hata hivyo aina ya mdalasini unaotumia pia inahusika katika kutibu kisukari au maradhi mengine. Nashindwa kupata maneno haya kwa Kiswahili lakini kuna aina kama mbili hivi za mdalasini ambazo ni ‘Cassia cinnamon’ ambao wenyewe huwa na kitu kingine ndani yake kiitwacho ‘coumarin’ ambayo ni sumu na husababisha matatizo katika ini. Mdalasini nzuri kwa kutibu kisukari na ambayo bei yake ipo juu kidogo ni ile iitwayo kwa kiingereza kama ‘Ceylon cinnamon’.
Namna ya kutumia mdalasini kutibu kisukari
• Chukuwa lita 1 ya maji na uyachemshe. Mara yatakapoanza kuchemka, ongeza vijiko 3 vikubwa vya mdalasini ya unga na uache kwa dakika kama 15 hivi kisha ipuwa chuja na unywe ikiwa bado ya uvugu uvugu kutwa mara moja kila siku kwa mwezi 1.
• Ongeza mdalasini kijiko kidogo kimoja cha chai katika kikombe kimoja (robo lita) cha maji ya uvugu uvugu, koroga na unywe kila siku.
• Unaweza pia kuongeza mdalasini ya unga ndani ya kachumbari kila unapokula.
3. MAJANI YA MANJANO
Utafiti unaonyesha kuwa, kutokana na kuwa na kiasi kingi cha madini kama vile madini ya chuma, Zinki, na shaba; majani ya manjano ni mhimu sana katika kuutunza usawa wa glukozi katika damu.
Madini haya huziamsha seli za kongosho zinazohusika na uzarishwaji wa homoni ya insulini. Majani ya manjano pia husaidia umeng’enywaji wa wanga mwilini. Yanao uwezo wa kuviamsha upya vimeng’enya katika figo na ini ambazo zinahusika katika kumeng’enya wanga na kuurudisha katika hali yake ya kawaida na hivyo kusaidia kutibu kisukari.
Wagonjwa wa kisukari huwa wana tatizo la kuwa na uwezo mdogo kudhibiti sumu mwilini jambo ambalo hupelekea seli zao za mwili kufa katika kiwango kingi. Utafiti unaonyesha kuwa majani ya manjano yana uwezo wa kupunguza kiasi cha seli kufa, seli ambazo ni mhimu katika uzarishwaji wa insulini.
Majani ya manjano yanaweza kushusha usawa wa damu sukari na ni mhimu sana kwa watu wanaopata kisukari kama matokeo ya uzito kuzidi. Ikiwa kisukari kinazunguka katika familia yenu, jitahidini kutumia majani ya manjano kwakuwa yamethibitika kuthibiti pia hata kile kisukari cha kurithi.
Namna ya kutumia majani ya manjano kujitibu kisukari
• Tafuna majani freshi ya manjano 7 mpaka 10 kila siku asubuhi.
• Tumia majani ya manjano kwenye kila chakula unachopika kila siku.
4. MSHUBIRI (Aloe Vera)
Wakati mshubiri umekuwa ukitumika kwa miaka mingi katika kutibu kisukari, baadhi ya tafiti za hivi karibuni zimeonyesha kuwa mshubiri unao uwezo pia katika kushusha kiwango cha damu sukari na mafuta katika mzunguko wa damu kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na kisukari. Mshubiri umethibitika katika kutibu kisukari cha aina ya kwanza na hata cha aina ya pili.
Jinsi ya kuandaa mshubiri kutibu kisukari
Changanya vifuatavyo:
• Jeli ya mshubiri kijiko cha chai 1
• Unga wa majani ya matunda ya damu ya mzee kijiko cha chai 1
• Unga wa manjano kijiko cha chai 1
Kunywa mchanganyiko huu kila siku kabla ya chakula cha mchana na jioni.
5. MAJANI YA MUEMBE
Wakati tunda la embe halina uwezo wa kutibu kisukari, majani ya mti wa muembe yanao uwezo huo! Waganga wengi wa Nigeria wamekuwa wakitumia sana majani ya muembe katika kutibu kisukari. Yanao uwezo wa kupunguza ufyonzwaji wa glukozi katika utumbo mkubwa hivyo kusaidia kupunguza usawa wa sukari katika damu. Pia yana uwezo mkubwa katika kudhibiti kiwango cha mafuta katika damu.
Namna ya kuandaa
• Loweka majani 10 mpaka 15 ndani ya nusu lita ya maji kwa usiku mmoja. Chuja maji haya asubuhi mapema na uyanywe kabla ya kula chochote. Subiri lisaa limoja lipite ndipo ule chakula cha asubuhi.
• Kausha majani ya muembe kwenye kivuli. Yatakapokuwa yamekauka kabisa, yasage kupata unga wake na hifadhi unga huu katika chombo kisafi na kisha lamba unga huu nusu kijiko kidogo cha chai kila siku kabla ya chakula cha mchana na jioni.
6. MREHANI
Mrehani (basil) una faida nyingi sana kiafya. Nje ya kudhibiti kisukari, Mrehani pia una sifa na uwezo katika kudhibiti asthma, kuondoa mfadhaiko, kudhibiti bakteria, kudhibiti virusi, kudhibiti vivimbe, kuondoa sumu mwilini, kudhibiti asidi tumboni, na kuongeza kinga ya mwili.
Mrehani huzisaidia pia seli za kongosho kufanya kazi zake vizuri na kusaidia utolewaji au uzarishwaji mzuri wa insulini.
Jinsi ya kuutumia mrehani kutibu kisukari
• Tafuna majani mawili mpaka manne ya mrehani kila siku asubuhi kabla hujala chochote.
• Ponda majani ya mrehani kupata juisi yake kama kijiko kimoja hivi cha chai na unywe kila siku asubuhi kabla ya kula kitu chochote.
7. BAMIA
Bamia zina kiasi kingi cha vitamini A, B6, C, K, magnesium, potassium, zinki, na faiba. Bamia ina uwezo mkubwa katika kusawazisha usawa wa sukari mwilini. Mbegu za Bamia zina kidhibiti kiitwacho alpha-glucosidase ambacho huzuia wanga kujibadili kuwa glukozi.
Faiba iliyomo kwenye bamia husaidia kurekebisha kiwango ambacho sukari humeng’enywa katika utumbo mkubwa.
Jinsi ya kutumia Bamia katika kujitibu Kisukari
Mahitaji:
• Bamia 2 mpaka 3
• Maji glasi 1
Jinsi ya kuandaa:
• Zisafishe bamia vizuri kabisa.
• Ondoa au ikate sehemu ya kichwa na mkia katika bamia na utupe. Kisha kata kila bamia katikati kwa urefu ili kupata vipande 2, hivyo utapata jumla vipande 4 kwa bamia hizo 2.
• Hivyo vipande 4 viweke ndani ya glasi iliyojaa maji, funika na uache hivyo kwa usiku mmoja.
• Asubuhi na mapema kunywa hayo maji yote yaliyokuwa na bamia kabla ya kula kitu kingine chochote. Ukiweza unaweza kula hata hizo bamia pia. Bamia mbichi zinafaida zaidi mwilini kuliko zilizopikwa.
Fanya hivi kila siku kwa miezi kadhaa.
8. MBEGU ZA KATANI
Mbegu za katani zina kiasi kingi cha mafuta mhimu sana yajulikanayo kama “essential omega-3 fat alpha-linolenic acid (ALA)’’, pia zina protini, faiba na muunganiko wa mmea uitwao ‘lignans’. Hii lignans hufanya kazi kama kiuaji sumu au kwa maneno mengine hufanya kazi ya kuondoa sumu mwilini. Baadhi ya tafiti zimeonyesha kuwa mbegu za katani zinao uwezo wa kusawazisha usawa wa damu sukari mwilini kwa vile zina kiwango kikubwa cha faiba ndani yake.
Mbegu za katani zinasaidia katika kazi za kumeng’enya chakula, pia husaidia katika ufyonzaji mzuri wa mafuta na sukari. Kama unatumia mara kwa mara hizi mbegu za katani, kiasi chako cha sukari chaweza kushuka hadi asilimia 28 kwa wakati mfupi.
Jinsi ya kutumia mbegu za katani katika kutibu kisukari
• Ongeza kijiko kikubwa kimoja cha unga wa mbegu za katani ndani ya glasi ya maji au maziwa na unywe wakati wa chakula chako cha asubuhi.
• Ongeza kijiko kidogo kimoja cha chai cha unga wa mbegu za katani katika nafaka zako unazotumia wakati wa chakula cha asubuhi.
• Ongeza pia unga wa mbegu za katani katika supu.
9. CHAI YA MAJANI YA MPAPAI
Majani ya mpapai ni mazuri katika kuongeza ufanisi wa insulini. Ni mazuri kwa watu wenye kisukari cha aina ya pili. Pia majani ya mpapai husaidia kupunguza matatizo yawezayo kuwatokea watu wenye kisukari, matatizo kama vile mafuta kwenye ini, matatizo katika kibofu cha mkojo na pia husaidia kupunguza mfadhaiko/stress.
Kuna faida nyingine kubwa zaidi ya kutumia majani ya mpapai ambayo ni uwezo wake katika kutibu vidonda vitokanavyo na kisukari kwa haraka zaidi.
Waganga wengi wa tiba asili kutoka Japani na Australia Na wengine wengi toka mataifa mbalimbali wamekuwa wakitumia majani ya mpapai kutibu kisukari kwa miaka mingi sasa.
Mahitaji:
• Majani 10 ya mpapai
• Maji lita 2
Maandalizi:
• Tumbukiza hayo majani ya mpapai katika maji.
• Chemsha hayo majani katika maji kwenye moto hadi maji yatakapobaki nusu yake (lita 1).
• Ipuwa na uache ipowe
• Kunywa maji haya kidogo kidogo kutwa nzima.
Fanya hivi kwa mwezi mmoja mpaka miwili.
Juisi hii ya majani ya mpapai iliyoandaliwa kwa mtindo huu ni nzuri katika kuondoa sumu mwilini na kurekebisha afya yako kwa ujumla huku ikirekebisha matatizo katika mfumo wa umeng’enyaji wa chakula na kuongeza kinga ya mwili wako.
10. JUISI MCHANGANYIKO YA ASILI
Hii ni juisi nzuri sana kwa mtu yeyote anayesumbuliwa na kisukari na hata shinikizo la damu, vitu vingi vinavyoingia katika juisi hii ni tiba nzuri kwa magonjwa mengi mwilini.
Hii ni juisi inayotengenezwa kutokana na mchanganyiko wa vitu tofauti vifuatavyo.
• Vitunguu swaumu 12
• Vitunguu maji 12
• Tangawizi 12
• Asali ya nyuki wadogo lita 1
• Ndimu 12
• Chumvi ya mawe kijiko kidogo kimoja
Namna inavyoandaliwa
• Saga (blendi) kwa pamoja vitunguu saumu na vitunguu maji pamoja na maji lita 2 na uchemshe kwenye moto kwa dakika kumi. Ikipoa chuja vizuri kupata juisi yake.
• Saga tangawizi pamoja na maji lita 1 Ikipoa chuja vizuri kupata juisi yake, weka pembeni kwenye bakuli safi
• Chukuwa limau au ndimu kata katikati kila moja na uchemshe kwenye moto na maji lita moja kwa dakika 15. zikishachemka subiri zipowe kisha zikamuwe na uchuje kupata juisi yake.
• Changanya hizo juisi zote hapo juu katika chombo kimoja kikubwa na kisha
• Ongeza asali ya nyuki wadogo mbichi nzuri lita moja, na mwisho ongeza chumvi ya mawe kijiko kidogo cha chai kimoja, koroga vizuri kwa pamoja.
Ukifuata vizuri maelezo haya mwishoni utapata juisi ya ujazo wa lita 5 au 6.
Kunywa juisi hii kikombe kimoja (robo lita) kutwa mara 3 kwa muda wa mwezi mmoja.
Juisi hii inaweza kukaa bila kuwekwa kwenye friji wiki 2 hadi 3 bila kuharibika.
VITU MHIMU VYA KUZINGATIA KWA MTU YEYOTE ANAYESUMBULIWA NA UGONJWA WA KISUKARI:
1. Acha kabisa soda ya aina yeyote pamoja na juisi za viwandani hadi hapo utakapopona
2. Acha chai ya rangi na kahawa
3. Jishughulishe zaidi na mazoezi
4. Ongeza unywaji maji na utumiaji wa chumvi hasa ya mawe ile ya baharini
5. Dhibiti uzito wako, hakikisha una uzito ule unaotakiwa kuwa nao kwa mjibu wa urefu wako
6. Tumia vyakula ambavyo havijakobolewa, mfano kama ni ugali tumia unga wa dona na siyo wa sembe n.k
Kama una swali liulize hapo kwenye comment sasa hivi.
Ikiwa unahitaji mojawapo ya hizi dawa za asili nilizozielezea kwenye hii makala niachie ujumbe mfupi (sms) kwenye 0769142586 au WhatsApp +18058551133, acha tu ujumbe nitakujibu na ninajibu haraka zaidi wale wanokuja WhatsApp.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top