Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Ndugu Gulam Husein (Picha Maktaba) |
Na Ezekiel Kamanga,Mbarali
Mkuu wa Wilaya ya
Mbarali, Mh. Gulamhussein kifu, aamuru
kukamatwa kwa Wenyeviti wa Vijiji pamoja na Watendaji wa Vijiji vya Kapunga (Kata
ya Itamboleo) na Ukwavila (Kata ya Mapogoro) kwa ajili ya uchunguzi wa
kusababisha migogoro ya Ardhi Wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali
amewaagiza Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) pamoja na Kamanda wa TAKUKURU Wilaya
kuwakamata Bwana Braithon Mwinuka Mwenyekiki
wa Kijiji cha Kapunga, Bwana Clement Mgaya Mwenyekiti wa Kijiji cha Ukwavila,
bwana Peter Kitta aliekuwa Mtendaji wa Kijiji
cha Kapunga na Bwana Naftal Fungo Mtendaji wa Kijiji cha Ukwavila kwa
kusababisha migogoro ya Ardhi, kugawa Ardhi bila ya kufuata utaratibu pamoja na
kusababisha kuuziwa watu tofauti kipande kimoja cha Ardhi.
Maamuzi hayo yametolewa
leo Desemba 12 kwenye kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama kilichojumuisha Watendaji
mbalimbali kutoka ngazi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Watendaji wa Kata
na Vijiji, Wenyeviti wa Vijiji na vitongoji pamoja na viongozi wa wafugaji
Wilaya ya Mbarali, kilichokuwa kinajadili kero mbalimbali zinazowakabili
wakulima na wafugaji.
Mh. Gulamhusein Kifu
vilevile amemuagiza Mkurugenzi Mtendandaji wa Halamashauri ya Wilaya ya Mbarali
kuhakikisha anachukua hatua stahiki na za haraka kwa Watendaji wote walio chini
yake watakaobainika kusababisha migogoro
katika maeneo yao.
Mwisho.
Post a Comment