Watuhumiwa wakifikishwa mahakamani . |
Pembe za Faru walizo kamatwa nazo watuhumiwa hao wanne rai wa China katika Mpaka wa Kasumulu Kyela. |
Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.Jamiimojablog
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mbeya imewahukumu kifungo cha
miaka 20 jela raia wanne wa China na kulipa faini baada ya kukutwa
na hatia kwa makosa matatu ikiwemo uhujumu uchumi kwa kukutwa na pembe za faru.
Kabla ya kuanza kusoma hukumu Hakimu mfawidhi Michael Mteite
alianza kuwashukuru Mawakili wa Serikali na Utetezi pamoja na Mkalimani Manfred
Lyoto kwa ushirikiano waliompatia na kuimaliza mapema kesi hiyo kwa siku 23 tu
ambapo ameweka historia yeye akiwa Hakimu Mfawidhi kwa kuimaliza kesi kwa muda
mfupi.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mahakama hiyo,
Michael Mteite aliyeanza majira ya saa tano asubuhi na kuahirishwa mara mbili
na kukamilika saa tisa na nusu alasiri ambapo alisema mahakama imeridhika
pasipo shaka kutokana na ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka
katika makosa yaliyokuwa yakiwakabili watuhumiwa hao.
Mteite alisema Mahakama ilijikita katika kiini cha makosa yote
matatu ambayo ni kupanga kutenda kosa kinyume cha sheria la uhujumu uchumi,
kufanya shughuli za nyara za serikali kinyume cha sheria ya utunzaji ya wanyama
pori inayosomwa pamoja na sheria ya uhujumu uchumi ambapo watuhumiwa waliingiza
pembe 11 za Faru bila kibali.
Alisema kosa la tatu ni kupatikana na nyara za serikali kinyume
cha sheria chini ya sheria ya uhifadhi ya wanyamapori inayosomwa pamoja na
sheria ya uhujumu uchumi ambapo maeklezo ya washtakiwa walikamatwa wakiwa
wanamiliki nyara za serikali bila kibali cha Mkurugenzi wa wanyama pori.
Hakimu Mkazi aliendelea kusema ingawa Washtakiwa weote kwa pamoja
walikana mashtaka lakini ushahidi upande wa Jamhuri uliuokuwa na mashahidi tisa
wate walieleza namna watuhumiwa walivyohusika na kosa hilo.
Alisema uchambuzi wa awali uliofanywa na Mahakama washtakiwa
walikubali kwamba wamesimama mahakamani wakikabiliwa kwa makosa matatu,
washtakiwa wa pili, tatu na nne walikubali kukamatwa Kyela mjini na kurudishwa
mpakani.
Kwa upande wake mwendesha mashtaka wa Seriakali Wankyo Simon
akisaidiwa na Archiles Mulisa walisema Washtakiwa hawana kumbukumbu ya makosa
ya nyuma ingawa makaso yao yanaonekana yalikuwa yakitendwa kwa kasi kubwa na
wanyama pori wamekuwa wakiathiriwa kiasi kwamba vizazi vijavyo vitakosa kuona
hazina ya wanyama kwa kuwa watakuwav wametoweka.
Alisema washtakiwa ni raia wa kigeni lakini walikuja nchini kwa
lengo la kufanya utalii katika Mlima Kilimanjaro lakini kumbe nyuma ya pazia
kuna jambo walikuwa wamelipanga hivy Mahakama inapaswa kutoa adhabu kali ili
iwe onyo kwa wengine wenye nia ya kufanya uovu kama huo.
Alisema Mahakama inapotoa adhabu izingatie kifungu cha 86,1,2 C
(ii) cha sheria ya Uhifadhi ya wanyama pori na kwenye kosa la tatu
izingatie kifungu cha 5 cha mwaka 2009 na kosa la kwanza kla uhujumu uchumi
izingatie sura ya 200 kwani wamevunja mkataba wa kimataifa wa kutunza wanyama
walioko hatarini kutoweka.
Alisema Mahakama pia izingatie kifungu cha 85 1(b) na (h) ya
sheria ya uhifadhi wanyama pori kwamba nyara zilizokamatwa zinakuwa mali ya
serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania sambamba na vifungu vya 111, 1(a),
(e) kwamba chombo kilichotumika kinataifishwa na kuwa mali ya Serikali sawa na
kifungu cha 111(4).
Pia Wankyo Simon ameiomba Serikali kupitia Mahakama kuwapa tuzo
watumishi wa umma waliowezesha kupatikana kwa nyara hizo na kuokoa raslimali za
Taifa wakiwemo Maafisa Forodha na Askari wa Jeshi la Polisi.
Aidha Mteite ameiambia Mahakama kuwa Gari namba T 103 DER mali ya
Mtuhumiwa wa kwanza Song Lei likabidhiwa Serikalini na simu za watuhumiwa
zitauzwa na Mahakama hiyo na nyaraka nyingine zitakabidhiwa kwa upande wa
Mashitaka.
Awali Wakili wa Utetezi Ladislaus Rwekaza aliiomba mahakama
kuwapunguzia adhabu washtakiwa kwa kuwa ni mara yao ya kwanza kutenda kosa, pia
ni raia wa kigeni pia ni vijana wadogo ambao ni nguvu kazi inayotegemewa na
taifa lolote.
Hakimu Mteite alisema katika hukumu yake amezingatia maombi ya
pande zote zote mbili na kwamba hakuna ubishi kuwa wanyama wanauawa na
kuisababishia serikali inaingia gharama kubwa kuhifadhi wanyama pori ili
kunusurui wanyama kutoweka.
Alisema katika kosa la kwanza la uhujumu uchumi washtakiwa
wanahukumiwa kifungo jela miaka 15 kila mmoja, kosa la pili kwa
mujibu wa kifungo cha 83,84(1) washtakiwa wataenda jela kila mmoja miaka 3 na
faini ambayo ni gharama ya mara mbili ya mali waliokutwa nao hivyo
watapaswa kulipa Dola za kimarekani 836000.
Alisema katika kosa la tatu kifungu cha 86, 2( c ) inawataka
washtakiwa kutumikia kifungo cha kuanzia miaka 20 hadi 30 lakini Mahakama
inawahukumu miaka 20 jela na kulipa faini ya fedha ambayo ni mara kumi ya mali
waliokutwa nayo ambapo watalipa dola za kimarekani 4180000.
Alihitimisha kwa kusema Washtakiwa kila mmoja atatumia adhabu zote
kwa pomoja ambayo ni miaka 20 samba mba na faini zilizoorodheshwa.
Alisema watuhumiwa wanahaki ya kukata rufaa kama wataona wameonewa
katika hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo.
Washtakiwa waliohukumiwa kifungo cha miaka ishirini ni pamoja
na Song Lei, Xiao Shaodan, Chen Jinlian na Hu Liang ambao walikamatwa
Novemba 6, mwaka huu mpakani Kasumulu Wilaya ya Kyela mkoani hapa wakitokea
nchi jirani ya Malawi.
Mwisho.
Post a Comment