Na Mwandishi
wetu,Mbeya
Shirikisho
la Vikundi vya wakulima wa Kahawa Mkoa wa Mbeya (SHIVIWAKA)limetoa kilio chao kwa serikali juu ya unyonywaji unoa fanywa na baadhi
ya Halmashauri kwa kuwakata wakulima
asilimia 5 kwa sehemu ya mauzo yao.
Pia wanasema kuwa Serikali
kutotoa ruzuku ya pemebejeo kwa wakulima,licha ya kuwepo kwa garama kubwa za
uzalishaji nako kukachangia wakulima wengi kukata tamaa kabisa ya
uzalishaji na kuamua kulima mazao
mengine.
Hayo
yamesema na Mwenyekiti wa shirikisho la Vikundi vya wakulima wa Kahawa Mkoa wa
Mbeya (SHIVIWAKA) Ndugu Edward Masawe
wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na
kubadilishanaa uzoefu katika masuala ya
utwala bora na uwajibikaji .
Amesema wakulima wadogo wa zao la kahawa
wamekuwa wakinyonywa kwa muda mrefu sasa hasa kutokana na wengi wao kutokuwa na
elimu stahiki juu ya uhakika wa soko pamoja na bei elekezi hivyo umefika wakati
sasa serikali ikaingilia kati suala hilo .
Amesema
changamoto nyingine wanayokutana nayo wakulima hao ni pamoja na kukosekana na kwa vitendea kazi sahihi kwa ajili ya zao hilo la kahawa hali
inayo pelekea mkulima kushindwa
kushindwa kumudu mahitahi halisi ya undelezaji wa zao hilo.
Mwenyekiti
huyo amebainisha wazi kuwa endapo serikali itaamua kuingia kati na kuzungumza moja kwa
moja wakulima hao kutasaidia kuibua na kufahamu changamoto wanazo kutananzo badala ya kuiachia jukumu
hilo bodi ya kahawa ambao nao wamekuwa kikwazo kwa wakulima hao.
Aidha
mmoja wa wajumbe wa bodi hiyo ya
SHIVIWAHAKA ambaye pia ni katibu wa Muungano group kutoka Utengule
–Usongwe Ndugu Zakaria Mwashitete amesema suala la bei halisi sokoni hali ambayo inatoa fursa kwa baadhi ya
wananunuzi wa kahawa kupanga bei yoyote wanayotaka hali ambayo inamuumiza
mkulima huyo.
Mwisho
Post a Comment